3.9.17

SanDisk imeleta memori kadi ya ukubwa wa GB 400.

BY net tamaduni

Kampuni ya Western Digitial inayomiliki biashara ya memori kadi za
SanDisk wametambulisha memori kadi hii mpya ya ujazo wa GB 400
katika onesho la IFA 2017 linaloendelea huko Berlin, Ujerumani

Baada ya uzinduzi wake ni muda mfupi inatarajiwa kuingia sokoni kwa
kiasi cha Dola za Kimarekani zipatazo 250 (Takribani *Tsh 560,000).*
Sifa ya memori kadi hii ni kwamba ina spidi ya UHS-1 yaani inaweza
kusafirisha 100MB/s ambapo ni sawa na picha 1,400 kwa dakika moja. Pia
inaweza kuhifadhi video ya masaa 40 yenye kiwango cha 1080p.

Memori kadi hii itawasaidia watumiaji Simu Janja na Kamera kuwa na uwezo
mzuri kuhifadhi vitu vingi kwa wakati mmoja.

Kwa sasa hii ndio memori kadi yenye ukubwa zaidi kuliko nyingine.
Memori kadi iliyokuwa inashikilia rekodi ya ukubwa ni ile
iliyotengenezwa na Samsung yenye ujazo wa uhifadhi wa 256GB.