29.1.17

Mambo 6 ya kuepuka kama wewe ni dereva wa Automatic Transmission Car

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.Teknolojia ya vyombo vya usafirishaji inabadilika kwa kasi sana kadri miaka inavyokwenda. Leo hii makampuni mengi yanayotengeneza magari yanazalisha magari mengi yenye uwezo wa kujibadilisha gia yenyewe (Automatic Transimission Cars) tofauti na hapo zamani.

Kuna tofauti kubwa sana ya kiutendaji kati ya magari haya ya automatic na yale ya manual. Magari haya ya automatic ni rahisi sana kuyaendesha kwa kuwa sehemu kubwa ya mfumo wa utendaji wake ni wa kisasa kabisa. Ila kuna vitu vya msingi usivyotakiwa kufanya wakati unaendesha magari haya ili kuongeza maisha ya gear box (Transmission Box).

1. Usipaki gari lako bila kubana Parking Brake

Mara nyingi madereva wamekuwa wakipaki magari yao kwa kuweka transmission handle kwenye herufi P, bila ya kuengege Parking Brake. Kama wewe ni mmoja wao tafadhali acha kufanya hivyo kwa sababu Parking Pawl, kichuma kinachoizuia gari kuondoka wakati imewekwa kwenye Park ni kidogo sana na hakijatengenezwa kwa kazi hiyo. Hivyo ikitokea mtu akaligonga gari lako kidogo kuna uwezekano mkubwa wa gari lako likaanza kutembea kama ulikuwa hujalizima. Pia kipande cha Parking Pawl kilichovunjika kinaweza kikaleta matatizo makubwa katika gear box yako.

2. Epuka kutumia Gear kubwa kama brake

Mara nyingi wakati unashuka milima mkali na gari ya manual huwa tunashusha gari katika gear kubwa kama namba 2 au 1 ili kupunguza kasi ya mwendo. Usijaribu kufanya hivyo kwa gari ya automatic transmission, kwa sababu itasababisha kuchubuka na kulika kwa vyuma vya ndani ya transmission box na kuleta usumbufu hapo baadae.

3. Usibadili Gear wakati mzunguko wa engine wa gari ni mkubwa

Kubadili gear wakati mzunguko wa engine wa gari lako ni mkali ni kitu kibaya kwa sababu itasababisha kulika kwa clutch plates za ndani ya gear box yako na kukuletea matatizo hapo baadae.

4. Usibadili Gear ya mbele kwenda ya nyuma moja kwa moja au ya nyuma kwenda ya mbele moja kwa moja bil ya kusimamisha gari kwanza

Simamisha gari lako kabisa kabla ya kuamua kubadili gear ya kutoka mbele na kurudi nyuma au vinginevyo. Kufanya hivyo bila kusimamisha gari lako kutapelekea uharibifu mkubwa katika gear box yako.

5. Hakikisha engine inapata joto la kutosha kabla ya kuanza kuendesha gari lako

Kama ulilipaki gari lako muda mrefu sana no bora ukaliacha kwa muda baada ya kuliwasha ili engine ipate joto la kutosha na kufanya vimiminika vyote vya katika gari kutawanyika na kufika katika maeneo husika katika kiwango stahiki.

6. Usipitishe muda wa kufanya service mara kwa mara

Wengi tumekuwa na tabia ya kupitisha muda wa kuyafanyia service magari yetu mara kwa mara. Maisha na ubora wa gari lako hutegemea sana muda wa service hasa kubadili oil za engine na transmission box, brake pads, air filter na vingine vingi.