6.2.17

Jifunze jinsi ya kutoa Pattern lock au Password katika Android Smartphone bila kupoteza data zako

BY net tamaduni

 Android ni mfumo endeshi unaotumika zaidi katika smartphones kwa sasa duniani kote na wahandisi (Engineers) kutoka google wanafanya kila linalowezekana kuifanya iwe na ulinzi na usalama wa kutosha  (secure) kila wanapotoa updates.

Kama nilivyoeleza katika makala iliyopita kuhusiana na ulinzi wa simu au kifaa chako cha android ni muhimu sana kuweka screen lock ili kuzuia wasiohusika na simu yako kutoitumia kabisa. Kuna njia nyingi zinazotumika kulock screen zetu ila maarufu ni zile za kuweka pattern lock, password au PIN.
Sasa ikitokea kwa bahati mbaya umesahau PIN, Password au Pattern inakuwa ngumu sana kutumia simu yako, wengi huwa wanafanya hard reset njiaya kutoa lock kwa kufuta kila kitu na kuanza upya. Inakuwaje kama una data au picha ambazo hutaki zipotee?, Hapo unakuwa mtihani kidogo, ndio maana leo swahilitech tumeamua kukuletea njia rahisi ya kuweza kufungua simu iliyolokiwa kwa pattern au password bila kupoteza data zilizomo ndani yake.

Njia ya Kwanza: Toa Pattern Lock bila kupoteza Data kwa kutumia Aroma File Manager

  • Download Aroma File Manager hapa au hapa.
  • Simu yako ya Android ambayo imelokiwa (locked Android phone) na pattern au password.
  • Memory Card inayoweza fanya kazi katika simu yako iliyolokiwa.
Hatua ya 1: Baada ya kudownload Aroma File Manager, iweke katika memory card yako, kumbuka kuweka katika root file (Root file ni pale unapofungua tu memory card yako na si ndani ya mafolder ya memory card). Weka memory card yako katika simu iliyolokiwa.
Hatua ya 2: Zima simu yako, subiri kwa sekunde thelathini ili izimike kabisa, washa simu yako kwa kushika batani ya kuwashia (power button) na batani ya kuongeza sauti (volume up button) kwa wakati mmoja ili kuingia katika Stock Recovery Mode, hapa inategemea na kampuni ya simu kwa sababu kila simu ina njia yake ya kuingia katika stock rocovery mode ili zilizo nyingi zinatumia njia hii.
Hatua ya 3: Baada ya kuingia katika Recovery Mode, tumia batani za sauti (volume buttons) kufanya machaguo huku volume down (batani ya kushusha sauti) ukitumia kushusha kivuli katika orodha na batani ya power ikitumika kuchagua (hapa pia inategemea na simu, batani ya kuongeza sauti inaweza ikatumika kufanya machaguo pia).
Hatua ya 4: Baada ya hapo chagua chaguo lililoandikwa  “Install Zip from SD Card” na chagua Aroma File Manager kwenye SD Card.
Hatua ya 5: Baada ya kuinstall itajifungua yenyewe kwenye recovery mode, shusha mpaka kwenye Settings ukiwa ndani ya Aroma File Manager, alafu shusha mpaka karibu na chini kabisa na chagua “Automount all devices on start” alafu exit.
Hatua ya 6: Rudia hatua ya 4 na isubiri mpaka ifunguke, Aroma File Manager itafunguka yenyewe tena. Sasa shuka mpaka kwenye Data Folder >> System Folder alafu tafuta “gesture.key” kwa pattern lock au “password.key” kwa password lock.
Hatua ya 7: Futa hayo mafaili kwa kutumia delete alafu restart simu yako. Baada ya kurestart utagundua pattern loki au password bado haijatoka, usiogope ingiza chochote au chora pattern yoyote na simu yako itafunguka ila kumbuka hiyo pattern uliyoichora hapo.

Njia ya Pili ya kutoa Pattern lock au Password bila kupoteza data kwa kutumia Android SDK Tools

Hatua ya 1: Download na kuinstall Android SDK Tools hapa. Chagua chaguo sahihi kulingana na Mfumo endeshi unaotumia kama ni Windows au Linux alafu install.
Hatua ya 2: Baada ya kuinstall, ifungue, uncheck (toa tiki) katika machaguo yote na acha Android SDK Platform-tools alafu bonyeza install packages kama picha hapo chini inavyoonyesha.
install-sdk-platform-tools
Hatua ya 3: Hakikisha USB Debuging ilikuwa ipo on kabla simu yako haijalokiwa, hakikisha pia una drivers sahihi za simu yako maana njia hii haitakuwa na maana kama huna drivers za simu yako.
Hatu ya 4: chomeka simu yako katika Pc/Laptop kwa kutumia USB Cable, fungua folder ulipoiweka install Android SDK Tools mara nyingi inakuwa hapa Users >> App Data >> Local >> Android >> Android-SDK >> Platform-Tools. Alafu click eneo lolote tupu hapo ndani, bonyeza shift alafu right click mouse yako na chagua “open command window here”. Itafungua command window na utaweka command zifuatazo hapo.
how-to-unlock-android-smartphone-pattern-lock-withou-data-losing
Angalia kama Kifaa chako kipo connected, alafu weka command kama zinavyoonekana katika picha.
unloack-android-pattern-lock-without-data-losing-command-image
Anza na hizi,
adb shell
cd /data/data/com.android.providers.settings/databases
sqlite3 settings.db
update system set value=0 where name=’lock_pattern_autolock’;
update system set value=0 where name=’lockscreen.lockedoutpermanently’;
.quit
Kama command hizo hapo juu hazitafanya kazi, tumia hizi,
   adb shell rm /data/system/gesture.key
Hatua ya 5: Baada ya kumaliza restart simu yako, itakapowaka utaona pattern au lock imejitoa yenyewe. Cha kuzingatia ili njia hii iweze kufanya kazi ni lazima USB Debuging iwe on kabla ya simu kulokiwa.

Tafadhali tumia njia hizi katika simu halali, usitumie njia hizi katika simu za wizi au ya mpenzi wako bila ridhaa yake.