30.8.16

JINSI YA KUWEKA APPS KWENYE SIMU ZA ANDROID BILA GOOGLE PLAY

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.Unamiliki tableti au smartphone inayokubali WiFi tuu na si kuweka laini, mtaani kwako hauna jinsi ya kupata WiFi, au kuna ugumu wowote umetokea kiasi ya kwamba huwezi kupata WiFi, je utawekaje apps kwenye tableti yako? Hii ni moja ya sababu ila kuna sababu nyingine mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu atake kuweka apps kwenye simu za android bila kutumia Google Play.
                
Leo Net tamaduni tutakuonesha jinsi ya kufanya hivyo, iwe kwenye simu
au tableti yako yoyote unayotumia programu endeshaji ya Android
njia hii itakusaidia kuingiza/kupakua apps bila kupitia soko la
Google Play.

Angalia sababu nilizoziandika apa chini kama moja wapo au zote
zinaendana na sababu inayokuzuia kupata app unayoitaji. Naelewa simu
nyingi za Android zilizopo sokoni kwa nchi zetu nyingi zikiwa kutoka kwa
makampuni yasiyo na jina kubwa sana unaweza kukuta hazijaja na soko la
apps la Google Play na hivyo ukajikuta unakosa apps mbalimbali.


Je kwa nini utumie njia hii?

* Wenye simu/tableti za Android ila hawawezi kupata huduma ya intaneti
kwenye vifaa hivyo
* Unalo solo la Google Play Store ila hauna akaunti ya Google/Gmail
inayokuwezesha kuingia kwenye soko hilo
* Unapata intaneti kwenye kifaa chako ila hauna app ya Google Play
* App unayoihitaji imeondolewa kwenye soko la Google Play kwa sababu
yeyote ile
* App unayoihitaji Google wameona haina sifa ya kuwa kwenye
simu/tableti yako na hivyo ukienda kwenye Google Play unaikosa app
hiyo ingawa kwa uhalisia inaweza kufanya kazi kwenye kifaa chako
* App unayoitaka inapatikana kwa ajili ya watumiaji wa nchi flani tuu
na hivyo kwa Tanzania au kwingine kokote haipatikani kwenye Google Play
* Au kwa sababu nyingine yeyote…

Njia itakusaidia kupakua apps za Android kwenye simu au tableti yako;
1. Bila kuwa na Google Play kwenye kifaa chako
2. Ata kama kifaa hicho hakina intaneti
3. Ata kama ujaweka akaunti ya Google kwenye simu/tableti yako

Vitu vya Kufahamu:

Kama vile programu za kompyuta za Windows zinaishia na .EXE basi jina
rasmi la apps za Android ni .APK, *kirefu cha APK ni Android Package
File*. Hivyo katika njia hii tutakukufundisha jinsi ya kupakua mafaili
ya APK kwenye simu au tableti yako.


Hatua ya Kwanza: Ruhusu Uwekwaji wa Apps Kutoka Sehemu Zisizo Rasmi

Kupitia mipangilio yake (settings), programu endeshaji ya Android huwa
hairuhusu apps kujipakua kwenye simu/tableti zake bila kupitia soko
spesheli mfano Google Play. Kuruhusu jambo hili nenda kwenye sehemu ya
’Settings’ ya simu yako, kisha ‘Security’ halafu bofya kutiki eneo la
‘Unknown Sources’. Itakuuliza kama unahakika na unachokifanya, bofya Ok.

Settings > Security> Wezesha ‘Unknown Sources

Pia kama chini ya eneo hili la ‘Unknown Sources’ utaona sehemu
imeandikwa *‘Verify Apps’,* na inatiki ondoa tiki hiyo. Kama sehemu hiyo
haipo basi tuendelee na hatua ya pili.

                 
(Hakikisha mara zote baada ya kumaliza kupakua app yako unarudi hapa na
kuondoa ‘tick’, patakulinda dhidi ya apps zitakazotaka kujipakulia apps
zisizosalama.)


Hatua ya Pili: Shusha Faili la App ya Android (APK) unalolitaka
Kutoka Kwenye Intaneti

Apps zote ata kwenye Google Play unapokuwa unaipakua huwa inakuja kwenye
mfumo wa APK, mfumo huu kama tulivyouelezea hapo juu ndio jinsi mafaili
ya apps ya Android hufadhiwa. Kwa kuwa atutatumia Google Play, basi
itabidi utafute faili hilo sehemu nyingine na hii inaweza ikawa kupitia
kivinjari kama cha Opera, Chrome au Firefox cha simu/tableti hiyo hiyo
au nyingine au ata kwenye vivinjari vya kwenye kompyuta.

Kuna mitandao mingi sana ambayo unaweza kupata mafaili ya APK yaliyo
salama kabisa kwa ajili ya apps mbalimbali. Njia rahisi ni kwenda Google
na kuandika ‘JINA LA APP UNAYOTAFUTA’ halafu unaongezea ‘APK file’,
mfano kama unataka kupakua app ya WhatsApp basi nenda Google na andika
‘WhatsApp APK file’ kisha bofya kutafuta.

*Sehemu za Kupata APK*


-Mtandao muhimu sana kwa usalama ni
*http://apps.evozi.com/apk-downloader/* . Kupitia mtandao huu wewe
unaenda kwenye soko la Google Play kwenye kompyuta yako, bofya eneo la
‘linki’ pale juu, ikopi na uiweke kwenye eneo la kutafuta kwenye huo
mtandao wa *EVOZI*, ukifanya bofya ‘Generate Download Link’ basi wao
watakupatia faili la APK la app hiyo mara moja kutoka Google Play na
utalishusha (download kwenye kompyuta yako.
              
                                                  Muonekano wa mtandao wa EVOZI

– *Mitandao mingine inayokuwezesha kupata mafaili ya APK kwa urahisi* ni
pamoja na *http://www.crackapk.com/*, *http://play.mob.org/
http://www.androidapksfree.com/ http://globalapk.com/* na mingine mingi
. Baadhi ya mitandao hii inatoa hadi apps zinazouzwa Google Play bure
kabisa (Ila hatukushauri utafute apps hizo 🙂 Kazi kwako!)


Hatua ya Tatu: Hamisha Faili Lako la APK kwenye Simu/tableti
unapotaka Kuiweka

Kama umeshusha faili la APK kupitia kivinjari cha simu/tableti yenyewe
basi hatua hii haiitajiki, ila kama umeshusha faili hilo kupitia
kompyuta basi itabidi kupitia ‘memori kadi’ au kwa kuchomeka waya wa USB
basi uhamishe faili hilo kutoka kwenye kompyuta na kuliweka kwenye simu
au tableti hiyo.


Hatua ya Mwisho: Bofya Faili Hilo la APK Kulipakua Kwenye simu au
tableti yako

Kwa kutumia app ya kusoma mafaili yaliyokwenye simu/tableti yako, basi
*nenda kwenye sehemu ulipoweka faili hilo la APK na ulibofye
kulifungua.* Kama umelishusha (download) kwa kutumia kivinjari cha
simu/tableti hiyo basi bofya tuu eneo la ‘notifications’ utakapoambiwa
limemaliza kushushwa kwa asilimia 100.

Ukilibofya faili hilo la APK litafunguka kama hapa chini; Bofya
‘Install’, kisha tulia na subiri, itachukua sekunde chache tuu faili
hilo kujipakua kwenye kifaa chako na katika kujipakua huku intaneti
haitahitajika kabisa. *UMEFANIKIWA!!!!*
               

*Njia hii inaweza kukusaidia ata kama pale ambapo una vifaa viwili vya
Android*, kwani badala ya kushusha app hiyo sehemu zote mbili kitofauti
tofauti na hivyo kutumia bando yako kwa mara mbili zaidi basi njia hii
itakusaidia kwani utalishusha faili mara moja tuu na kuweza kulitumia
kuweka app hiyo kwenye vifaa vyako vyote.


Je ushawahi kutumia njia hii? Na kama bado je unadhani itakusaidia
kwa kiasi gani?