30.8.16

FAHAMU SIFA,UWEZO NA BEI YA SIMU TECNO Boom J8!

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.Tecno Boom J7 ilipokelewa vizuri sana kutokana na ubunifu na upatikaji wake katika bei iliyokuwa ya nafuu ukilinganisha na simu zenye sifa kama

yake kutoka makampuni mengine.Sasa ni Boom J8 watoto wa mjini wanasema ni habari ingine kabisa.Fahamu uwezo wake, muonekano wake n.k 
Tecno Boom J8Simu ya Tecno Boom J8 pamoja na Headphones zake

Ni nini cha kipekee zaidi katika Tecno Boom J8?
Kwanza – TeknoKona tunaweza chambua matoleo makuu matatu ya simu za
Tecno kama ifuatavyo; kuna zile zinazolenga soko la bei ya juu – Tecno
Phantom, kuna zile kwa ajili ya watumiaji wa aina zote, Tecno Camon, na
hizi za Tecno Boom – ambazo zinalenga watu wa kisasa zaidi, wapenzi wa
muziki na mambo ya kisasa.

*Sifa/Uwezo wa Boom J8 kwa ufupi*

* Programu endeshaji: Android 5.1 spesheli ya HiOS
* Teknolojia za mawasiliano: 2G/3G/4GLTE (GSM/WCDMA/LTE) ( LTE:Band
B3/7/20)
* Prosesa: Quad-core
* Kioo (Display): Inchi 5.5 HD IPS Touchscreen
* Kamera: Megapixel 13 nyuma, MP 5 mbele (selfi), zote zinapiga Flash
* Diski ujazo (storage): GB 16GB pamoja na RAM ya GB 2
* Uwezo wa betri: mAh 3000
* Teknolojia zingine – Wi-Fi, BT, GPS
* Unaweza tumia memori kadi (Micro SD) ya hadi GB 128


Android 5.1 – HiOS

Simu hii inakuja na toleo la programu endeshaji la Android 5.1 lakini
lilofanyiwa maboresho ya muoneakano uliopewa jina la HiOS. Muonekano huu
wa HiOS ukijumlisha na RAM ya GB 2 iliyokwenye simu hii inaifanya simu
hii kuwa na kasi nzuri katika utendaji wake.
hiOSHiOS, utaweza kupata masasisho (updates)

Na kama katika matoleo yake ya simu zake za sasa, Tecno wameweka *mfumo
wa kuendelea kupata masasisho (updates)* kwa simu hii. Baada ya
kuunganisha na intaneti nilipata taarifa (notification) ya kwamba
natakiwa kuupdate.


Muonekano

Ukiishika kwa mara ya kwanza lazima utakubali ya kwamba simu hii ni
maboresho makubwa kutoka Tecno Boom J7. Boom J8 ni nyembamba na
inastahili sifa ya kuwa kati ya simu janja nyembamba zaidi za ukubwa wa
inchi 5.5.

Kutengeneza kasha lake (housing) imetumika plastiki pamoja na aluminiamu
ambayo inasaidia kuipa simu muonekano wa kuvutia.


Kamera

Kwenye Tecno Boom J8 kuna maboresho kadhaa kutoka toleo la J7. J8
inakuja na kamera ya nyuma ya MP 13 na ya selfi MP 5, ukilinganisha na
J7 ambayo ilikuwa na kamera ya nyuma ya MP 8 na ya selfi ikiwa ni MP 2.
simu ya tecno boom j8Picha iliyopigwa kwa kutumia simu ya Tecno Boom J8
Hii ni Morogoro

Kamera zimekuja na teknolojia ya maboresho ya ubora wa picha – optical
image stabilization. Pia kamera ya nyuma inauwezo wa kupiga picha za
panorama. App ya kamera inauwezo wa kutambua (‘detect’) sura na pia
inakupa nafasi ya kuboresha vitu kama mwanga n.k kabla ya upigaji picha.

Ukaaji wa Chaji (Betri)

Katika majaribio niliyofanya nilifanikiwa kuangalia muvi mbili kupitia
app ya VLC niliyoipakua pamoja na kusikiliza muziki kwa zaidi ya masaa
mawili na bado nikawa na kiwango cha chaji cha zaidi ya asilimia 40%.

Tecno *Boom J7 ilikuja na betri ya mAh 2020 wakati Boom J8 imeongezwa
maradufu kiwango cha betri na kufikia mAh 3000.* Kwa kipimo hichi
utaweza kufanya mambo mengi ndani ya siku bila ya kuwa na wasiwasi na
suala la chaji. Pia kupitia uwezo wa *‘Ultra lower power mode’* utaweza
kufanya simu yako kutumia kiwango kiduchu zaidi cha chaji kwa apps
muhimu tuu pale unapojua utakuwa mbali na uwezo wa kuchaji kwa muda mrefu.

Muziki na Boom Player
Tecno Boom J8 Boom PlayerMuonekano wa sehemu zote za app ya Boom Player

App ya Boom Player ni moja ya kitu kilichoboreshwa zaidi katika simu ya
Tecno Boom J8. Kwa muda mrefu app ya Boom Player ilikuwa kama app
nyingine yeyote ya kawaida ya kusikilizia muziki, lakini kwa sasa app ya
Boom Player imepewa uwezo mkubwa zaidi.

*Sifa/uwezo wa App ya Boom Player*

* *Kusikiliza muziki uliyohifadhi kwenye simu yako* (au kupitia memori
kadi yako – na video pia)
* Kusikiliza*nyimbo mbalimbali za kimataifa na za Tanzania* kupitia
njia ya ku’stream
* Pia *tazama video* ulizohifadhi kwenye simu yako
* Tazama pia *video za nyimbo mbalimbali za kimataifa na za Tanzania*
kupitia njia ya ku’stream
* Utaweza pia kushiriki katika mazungumzo juu ya wimbo au video flani
na watumiaji mbalimbali wa app hiyo kutoka nchi zingine wanaotumia
app hiyo
* Utaweza kulike na kushare nyimbo unazopenda n.k kwenda kwenye
mitandao ya kijamii kama vile Facebook
* Kudownload nyimbo kabisa kabisa itabidi ulipie

Ingawa ukinunua simu hii inatakiwa pia kupewa headphone za bure ila bado
kupitia app ya *Boom Maxx* utaweza kuchagua mipangilio ya sauti
kulingana na aina ya earphones/headphones unazotumia.

*App ya Boom Player imeunganishwa vizuri na simu kiasi ya kwamba
ukiwa unasikiliza muziki basi kuna eneo la chini tu baada ya display
litakuwa linawaka waka kutokana na jinsi mdundo wa muziki unavyopiga.*

[Soma Pia ->Kuhusu shindano linalohusisha Boom Player ambalo mshindi
atapelekwa nchini Ufaransa katika jiji la Paris
<http://teknokona.com/2016/05/10/paris-boom-j8-tecno-tanzania-waja-na-shindano/>}

*Na majaribio tuliyofanya ya kusikiliza mzuki kupitia Boom Player na
pia app zingine kama vile Shuttle na DeaDBeef ambazo ni moja ya apps
nzuri kabisa za bure bado tuligundua kuna ubora flani nyimbo
zinasikika vizuri zaidi kwenye Boom Player.*

Tecno Boom J8 pia imetengenezwa kwa teknolojia za juu za mfumo wa sauti
– hivyo iwe kupitia spika za simu yenyewe au pale unapotumia headphones
kiwango kizima cha sauti kinachotoka ni cha kiwango cha juu. Boom Player
kama app spesheli ya simu hii ipo katika uwezo mkubwa wa kutumia
teknolojia hizi kuhakikisha kiwango cha uchezaji muziki ni cha juu.


Bei:
Wakati Boom J8 imekuja na maboresho mengi bado bei yake haijaenda mbali
sana na ile iliyokuja na Boom J7, *simu ya Boom J8 inapatikana kwa kati
ya Tsh 380,000/= hadi Tsh 450,000/=, hivyo kama ni bajeti basi ukiwa na
Tsh 400,000 unaweza ukawa poa. (Kwa Kenya Ksh 14,999/- Ksh 16,999/=)*

Uchambuzi umekuwa mrefu kutokana na upatikanaji wa simu hii na hivyo
kupata muda mrefu wa kuitumia vizuri.

Je umeshatumia simu ya Boom J7? au J8? Tuambie mtazamo wako juu ya
maboresho yaliyokuja katika Boom J8. Na usisite kutuambia simu
gani nyingine ungependa kuifahamu kwa undani.