30.8.16

JINSI YA KUZUIA WHATSAPP KUTUMA DATA ZAKO KWENDA FACEBOOK

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.Hivi karibuni tuliandika kuhusu WhatsApp kutuma data za watumiaji wake kwenda mtandao wa Facebook.Kama sehemu ya kutokwenda nje ya sheria WhatsApp wanakupa uwezo wa kukataa suala hilo ndani ya siku 30.


Inakuwaje?
Kama bado haujapata ombi la kukubali mkataba (Terms and Privacy Policy)
mpya kutoka WhatsApp basi unaweza pata muda wowote.Ingawa hakuna eneo la kukataa makubaliano hayo ila kuna kanjia karefu ambacho WhatsApp wanajua wengi hawatafuata ili kuwawezesha kukataa utoaji wa taarifa zao za utumiaji wa WhatsApp kwenda Facebook.

Hatua za kufuata
Hapa chini ni muonekano wa mkataba huo wa Terms and Privacy Policy
unavyoonekana pale unapokujia kwenye app ya WhatsApp.
                                          



Kuikatalia WhatsApp

Usibofye eneo la kukubali*‘AGREE’*, bali bofya eneo la chini la *“Read more about the key updates to our Terms and Privacy Policy.”* , ukibofya hapo maelezo zaidi yatafunguka na pia kuna eneo utaliona lishapigwa vyema (tick) likiruhusu WhatsApp kutuma data zako kwenda Facebook. *Ondoa tiki (vema) halo na kisha kubali.*
                                           


Kama ulishakosea na kukubali mkataba huu bila ya kuondoa hili basi
unaweza kusahihisha kwa kutembelea eneo la settings – Account Menu,
baada ya hapo ondoa ‘vyema’ kwenye enero la Share my account info.