30.1.17

Vitu 6 usivyotakiwa kufanya wakati unaendesha gari ya Manual (Manual Transmission Car)

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.Kuendesha gari la manual sio ngumu sana kama baadhi ya watu wanavyodhani. Pale linapokuja suala la kuendesha gari la manual, ni mchanganyiko wa usanii na sayansi ya mikono na miguu kwa pamoja.

Pale unapoendesha gari ya manual ile gear lever inawezekana ikawa kama kitu kigumu kwako, lakini unapoizoea ni kitu cha kufurahisha na starehe kucheza nacho hasa unapokuwa barabarani. Kuna baadhi ya mambo ya kuzingitia kabla au hata baada ya kujua kuendesha gari ya manual ili kujiweka salama barabarani na kukilinda chombo chako.

1. Kamwe usitumie gear lever kama egesho la mkono wako

                                manual-01
Tunaiona gear lever na kuitumia bila kujua nini kinafanyika nyuma ya pazia. Pale tunapotumia gear lever kubadilisha gear, selector fork ambayo huwa haizunguki huwa inakandamizwa kwenye collar inayozunguka na ile collar huwa inagandamizwa kwenye gear plate unayotaka kubadilisha. Kuweka mkono kwenye gear lever kwa muda mrefu kunasababisha kusagika kwa ile selector fork taratibu na kupunguza urefu wa maisha yake.

2. Usikanyage Clutch wakati gari linapoteremka katika mteremko ili kuongeza mwendo

                                 manual-03
Kukanyaga clutch wakati gari linateremka kwa kasi mteremkoni sio jambo la kufanya wakati unaendesha gari la manual. Hii itachangia sana kusaga baadhi ya maeneo katika mfumo wa gear wa gari lako. Pia itapelekea gari lako kukosa balance wakati wa kushuka katika mteremko. Cha kuzingatia ni makadirio ya mwendokasi, gear uliyopo na muda wa kuachia clutch husika.

3. Usiweke mguu wako muda wote juu ya pedeli ya Clutch

Kuweka mguu wako muda wote kwenye pedeli ya clutch kutaifanya clutch yako kuengage partially na kusababisha kutereza kwa clutch kila mara. Hii inapelekea kusagika kwa clutch na muda mwingine kunapelekea kupoteza kiasi kikubwa cha mafuta kwa sababu ya kupoteza transimission energy kubwa.

4. Usikanyage Pedeli ya Accelerator mpaka mwisho pale unapokuwa kwenye gear ndogo


Kukanyaga pedeli ya Accelerator (mafuta) mpaka mwisho pale gari lako linapokuwa katika mwendo mdogo sio vizuri kwa sababu kutapelekea kutumia kiasi kikubwa cha mafuta bila sababu. Unashauriwa kukanyaga pedeli yako ya mafuta mpaka mwisho pale tu unapokuwa katika gear za kasi ili kulifanya gari lako litembee katika mwendokasi mkubwa.

5. Usibadili Gear bila kukanyaga clutch

                                manual-04
Clutch inasaidia kutenganisha injini na gear box kila muda inapokanyagwa. Ni muhimu kukanyaga clutch kwanza kabla ya kujaribu kubadili gear yoyote ili kuipa maisha marefu gear box yako. Clutch Unit hutumika kusafirisha mzunguko wa injini kutoka kwenye injini kwenda kwenye transmission.

6. Usibane brake wakati wa kusimama bila ya kukanyaga Clutch

Wakati unapotaka kusimama ni muhimu sana kukanyaga clutch. Cha kuzingatia hapa ni muda wa kubana clutch, jaribu kupunguza mwendo mpaka pale unapoona sasa unahitaji kusimama na hapo unaruhisiwa kukanyaga clutch na kulifanya gari lako kusimama.
Kumbuka Clutch ni kila kitu linapokuja suala la gari za manual, hakikisha umepata mafunzo ya kutosha kabla ya kuanza kutumia gari la manual katika barabara kuu.