3.9.17

Rasmi: Uzinduzi wa iPhone 8 kufanyika Septemba 12 mwaka huu

BY net tamaduni

Baada ya tetesi nyingi za lini kampuni ya Apple itafanya uzinduzi
wa iPhone 8, toleo la simu yake mpya sasa rasmi wamethibitisha
kwamba uzinduzi utafanyika Septemba 12, 2017.

Uzinduzi huo utafanyika katika Huko Cupertino, California katika ukumbi
wa Steve Jobs, ambapo ni mara ya kwanza kufanyika hapo kwa tukio kama hilo.
Tukio hilo la Septemba 12 mbali na iPhone 8 linatarajiwa kutangazwa kwa
iPhone 7s, iPhone 7s Plus, Apple Watch 3 na 4k Apple TV.

Wakati uzinduzi wa iPhone 8 ukisubiriwa kwa hamu kubwa, sokoni tayari
kuna Samsung Note 8 ambayo inategemewa kuleta usumbufu kwa mauzo ya
iPhone 8.

Septemba 12 inaangaliwa kama siku ya Apple. Endelea kufuatilia
Net tamaduni kujua yatakayojiri siku hiyo.