3.9.17

Sababu 8 kwanini blog nyingi za kitanzania hufa?

BY net tamaduni

Blog ni jukwaa maarufu sana la kutolea na kupata taarifa na
      maarifa mbalimbali kwenye mtandao. Hivi leo mambo mengi
      tunayoyasoma kwenye mtandao yapo kwenye blog mbalimbali.
      Hivyo basi blog ni jukwaa linaloweza kutumiwa kueneza habari,
      maarifa pamoja na kujiingizia kipato.

Kwa kulifahamu hili watanzania wengi wamekuwa wakianzisha blog lakini
zinakufa au hazifanikiwi jinsi walivyotarajia. Ni vyema ukafahamu kuwa
yapo mambo yanayosababisha blog nyingi za kitanzania kufa; hivyo soma
mambo haya 8 hapa chini.

    1. Kuanzisha blog kwa lengo kuu la kupata pesa

Ni lazima utambue kuwa pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu au kumpa
mtu kitu au maarifa yenye manufaa kwake. Wamiliki wengi wa blog wa
kitanzania hawana lengo tofauti la kuanzisha blog zaidi ya kulenga
kupata pesa. Hii ndiyo sababu mtu anafungua blog leo kesho anaweka
matangazo kuwa “tangaza nasi hapa”. Nani atatangaza na wewe wakati una
watembeleaji 2 kwa siku? Ni lazima ujue kuwa kupata pesa kwenye blog ni
lazima ukubali na uwe tayari kulipa gharama ya kufanya kitu chenye
manufaa kwa watu.


    2. Ubinafsi

Ubinafsi ni tatizo linaloua mambo mengi mazuri ya watu, yakiwemo blog.
Watanzania wengi hawapendi kuwashirikisha watu wengine mawazo yao ili
washirikiane kwa pamoja kuyatimiza. Ikiwa wewe una wazo fulani kuhusu
blog, kwanini usimshirikishe mtu anayeweza kukusaidia mkatimiza wazo
hilo? Vivyo hivyo kwa wanaoshirikishwa wengi hawapendi kufanyia kazi
wazo lililoletwa na mtu mwingine. Wengi huliiba au kulinakili au hata
pengine kulikwamisha tu.

    3. Kulenga tu kupata watembeleaji (traffic) wengi

Wasomaji au watembeleaji hawaji tu kwenye blog yako kwa sababu unataka
waje. Ni lazima kuwa na kitu au sababu inayowafanya watembelee blog
yako. Ni lazima kabla hujawaza kuongeza watembeleaji kwenye blog yako
ukaandaa vitu vyenye manufaa makubwa kwao. Kamwe, injini pekuzi kama
Google na Bing havitoweza kuonyesha blog yako kwa watu kama haina kitu
cha maana. Kutokana na jambo hili wengi hujikuta wakishindwa kupata
watembeleaji kama wanavyotaka na kujikuta wakiacha kuendeleza blog zao.


    4. Kunakili machapisho kutoka blog nyingine
Huu ni ugonjwa mkubwa unaozikabili blog nyingi za kitanzania hasa zile
za habari. Habari ikishaandikwa kwenye blog moja, utaikuta kila mahali
iko hivyo hivyo. Ni wazi kuwa injini pekuzi kama Google inafahamu makala
iliandikwa wapi kwanza; hivyo huzichukulia blog nyingine zilizonakili

Kama unataka kuona matokeo mazuri ni lazima ukubali  kutoa jasho uandike
makala zako mwenyewe ambazo zitakupa manufaa makubwa.


    5. Kutokuwekeza gharama stahiki


Kama nilivyotangulia kusema, blog ni kazi inayohitaji kuwekeza gharama
fulani ili uweze kuona matokeo mazuri. Ni lazima uwekeze fedha na muda
ili uweze kufanikiwa katika kazi hii. Gharama ya muda na kujitoa ndiyo
inayohitajika zaidi kwenye blog. Utahitaji muda wa kutosha kuandaa
makala (post) zenye tija kwa wasomaji wako. Muda huu utahusisha
kutafiti, kupanga, kuandika na kuhariri machapisho yako ili yawe bora
kwa wasomaji.

    6. Kupuuza maarifa ya usanifu mtandao (web design)

Usanifu mtandao hauwezi kutengwa na blog. Kama unataka kuwa blogger
mzuri ni lazima uwe pia unafahamu jinsi ya kutumia programu mbalimbali
zitakazokuwezesha kutengeneza blog nzuri ambayo ni rafiki pia kwa
wasomaji na vifaa vyao. 
      Manufaa ya kutengeneza blog nzuri:
  •    Blog yako itaonekana ni rasmi na ya kitaalamu.
  • Injini pekuzi zitaifurahia na kuiweka juu zaidi kwa wasomaji wengi.
  • Itakuwa rafiki kwenye vifaa kama simu, tablet na kompyuta
Kama huna maarifa ya kusanifu blog, unaweza ukajifunza kwani ni rahisi.
Pia unaweza ukatumia watu na kampuni mbalimbali zinazofanya huduma hiyo
kwa bei nafuu.Mwonekano

    7. Kukata tamaa na kukosa uvumilivu
Mambo mazuri yana milima na mabonde yake. Hili liko wazi pia kwenye
blog; ikiwa unataka kufanikiwa kwenye blog basi ni vyema ukajifunza
kutokata tamaa na kuwa mvumilivu. Watanzania wengi wenye blog wanakata
tamaa pale wanapoona mambo hayaendi kama walivyopanga, huona kuwa blog
hailipi wala haina manufaa na kuachia njiani. Lakini ni muhimu
ukatafakari kuhusu tovuti kama Net tamaduni; je ilianza usiku mmoja?
Naamini Ndugu Elibariki wa Net tamaduni anafahamu milima na mabonde
waliyopitia kwa miaka kadhaa hadi kufika hapa ilipo leo. Jambo lolote
zuri linahitaji kuvumilia na kufanya kwa moyo.

    8. Makala duni
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kuwa watanzania wengi ni wavivu na
hawapendi kusoma. Labda hili ndiyo sababu hata bloggers wengi wa
kitanzania hawako tayari kujifunza jinsi ya kuandika makala nzuri kwa
ajili ya wasomaji na injini pekuzi. Ni vyema ukafahamu mambo muhimu ya
kuzingatia kwenye kila makala unayoiandika kama vile:

*Hitimisho*
Naamini sasa umefahamu kwanini watanzania wengi hawafanikiwi kwenye
blog. Ni wazi kuwa blog ni kazi kama kazi zingine, hivyo inahitaji
marifa stahiki na kuifanya kwa dhati. Naamini kama una blog au una
mpango wa kuanzisha ya kwako hutokwamishwa tena na mambo tajwa hapo juu.