2.4.16

SOMA HISTORIA JUU YA LOGO YA APPLE NA KWANINI IMENG'ATWA.!

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.Moja katika maswali mengi ambayo watu wanajiuliza kutoka katikalogo ya Apple ni kwamba kwa nini logo hiyo imeng’atwa upande mmoja?
Moja kati ya sifa kubwa katika kampuni la Apple ni kuwa na ubunifu wa
hali ya juu katika bidhaa zake ambao unatofautisha bidhaa za Apple na
bidhaa zingine nyingi. Kazi kubwa ya bwana Steve Jobs ilikuwa imejikita
sana katika ubunifu wa vifaa ukilinganisha na teknolojia. 
                   

Logo hiyo ina tunda la tufaha (Apple) ambalo kwa upande wake wa kulia
kuna kipande hakipo (kimeng’atwa), lakini kwa nini logo hiyo iko hivyo?
Mtu ambaye alitumika katika kutengeneza logo ya kampuni hiyo ni Bw. Rob
Janoff na sababu kubwa aliyoamua kuifanya logo ya kampuni hiyo kuwa na
tufaha (apple) ambalo halina kipande sehemu moja ni kwa kuwa alitaka
kulitofautisha tunda hilo na tunda la cheri (cherry)


Muundo Wa Tunda La Tufaha (Apple)


Tunda La Cheri (Cherry)

Hiyo ndio sababu kubwa lakini ngoja tuangalie katika logo zingine za
mwanzo jinsi zilivyokuwa kabla yah ii inayotumika sasa 


1. Logo Ya Kwanza 


Logo Ya Kwanza Ya Kampuni La Apple


Logo ya kampuni ya mara kwanza kabisa ilikuwa imetengenezwa spesheli
katika kumuenzi gwiji la sayansi Bw. Isaac Newton hasa pale alipogundua
uvutano (gravity). Logo hiyo ilimuonyesha Bw. Isaac amekaa chini ya mti
ambapo mti huo una tunda la tufaha (Apple) ambalo linawaka. Katika logo
hiyo kuna usemi ambao umeandikwa
Newton…A Mind Forever Voyaging Through Strange Seas of Thought…Alone
tafsiri ya haraka haraka ni kwamba “Akili inawaza mambo mbali mbali
ikiwa anaewaza yuko peke yake”
Japokuwa logo hii ilikuwa ni ya aina yake, lakini ilikuwa na mambo mengi
sana na mtu wa tatu kati ya wale wa kwanza kabisa katika kugundua
kampuni la Apple, Bw. Ronald Wayne aliliona hilo. Bw. Ronald Wayne baada
ya muda aliamua kuuza hisa zake (10%) za kampuni hiyo kwa dola za
kimarekani 800 cha ajabu ni kwamba kama anagekuwa na hisa hizo mpaka
sasa angekuwa na utajiri zaidi ya dola bilioni 2 za kimarekani 


2. Logo Ya Pili 


Logo Ya Pili Ya Kampuni La Apple 


Kampuni likaamua kutengeneza logo nyingine ambayo itakuwa ya aina yake
na ambayo itaweza kumvutia mtu. Logo hii ilitengenezwa mwaka 1977 na pia
ilitengenezwa na Bw. Ronald Janoff ambapo ilikuwa imeongezewa rangi.
Kampuni liliamua kuongeza rangi katika logo ya kampuni ili mradi tuu
kujiweka karibu na kuvutia macho ya wateja wao. Kitu kingine cha aina
yake katika logo hii ni kule kung’atwa kwa upande mmoja wa tunda. Logo
hii ilitumika katika bidhaa zote kutoka kampuni la Apple mpaka mwaka 1998. 


3. Logo Ya Tatu

Kwa kipindi cha mwaka 1998 mpaka mwaka 2007 kampuni la Apple lilizindua
logo 3 ambazo zinafanana (hazikuwa na tofauti kubwa ndani yake). Jambo
hili linazifanya logo hizi kuonekana kama moja tuu yenye maboresho kidogo
 

Logo Ya Tatu Ya Kampuni La Apple Kuanzia Mwaka 1998 Mpaka 2000 

Katika mwaka 1998 logo ya rangi ya blue ilizinduliwa kutokana na
kuachiwa kwa kompyuta za iMac. Logo hii ilianza kutumiwa baada ya Steve
Jobs kurudi katika kampuni hilo na iliachwa kutumiwa mwaka 2000. 


Logo Ya Tatu Ya Kampuni La Apple Kuanzia Mwaka 2000 Mpaka 2002
Kutoka mwaka 2000 mpaka 2002 Apple waliamua kuwa na logo nyingine
ambayo iko kawaida sana katika muonekano na staili ya kawaida sana. Hii
iliipelekea kampuni ya Apple kuwa na logo flani hivi ya kawaida yenye weusi mzuri. 



Logo Ya Tatu Ya Kampuni La Apple Kuanzia Mwaka 2002 Mpaka 2007

Kutoka mwaka 2002 na kuendelea Apple walitumia logo nyingine ambayo iliambatana katika uzinduzi wa Os ya Panther OS. Logo hii iliendelea
kutumiwa mpaka mwaka 2007 ambapo ndipo iPhone ya kwanza ilizinduliwa. 


4. Logo Ya Nne 


Logo Ya Nne Ya Kampuni La Apple Kuanzia Mwaka 2007 Mpaka Hivi Sasa

 Kuanzia mwaka 2007 logo ambayo haikuwa narangi ilianza
kutumiwa. Logo hii ilikuwa na mantiki kama ya glasi na usilva ndani yake. 


Hiyo ni stori fupi ya kampuni la Apple katika logo yake. Ni kitu kizuri
sana walichokifanya kampuni la Apple kwani makampuni mengi huwa
wanabadilisha kabisa logo zao pale wanapoona wanahitaji kubadilika
katika utendaji na kila kitu. Kampuni la Apple limeweza kuwa na logo
moja (japo wamefanya marekebisho madogo madogo) kwa kipindi cha muda mrefu. 
 Asante.
Endelea kutembelea Net TAMADUNI Blog kwa habari nyingine nyingi.