31.3.16

Jinsi Ya Kujitoa Kwenye Group la WhatsApp Na Kulivunja (kulifuta) Kwa Siri!

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.WhatsApp licha ya kutuleta kwake karibu lakini bado kuna vitu
vingine vinaboa katika mtandao huo kama ma’Group’ yasiyoeleweka.

Je ufanye nini? :-)
Utakuta ndani ya WhatsApp ‘Group’ moja lina watu kibao na wanaongea vitu
tofauti tofauti na kibaya zaidi wawe wameku Add tuu bila idhini yako.
Hii sasa haitakuboa bali itakukasirisha. Au kama uko kwenye ‘Group’
ambalo sio zuri ki maadili labda vitu vinatumwa na kupokewa na watu wa
kundi hilo havina maadili hapo vinaweza kukuharibia siku yako.
 

*Sasa basi kama unataka kujitoa katika Group ndani ya Mtandao wa
WhatsApp bila ya watu wengine katika lile ‘Group’ kujua kama umejitoa,
kuna njia spesheli ya kufanya hivyo.* Katika kutumia njia hii pia
utalazimika kuliharibu ‘Group’ kabisa kwani baada ya wewe kujitoa kwa
njia hii, ‘Group’ halitaweza kufanya kazi kabisa (litakuwa limeharibika) 

Tuifahamu Njia Hiyo
* Cha kwanza kabisa itakubidi utumie huduma ya WhatsApp ya kwenye
mtandao yaani WhatsApp Web

* Net TAMADUNI inashauri utumie kivinjari cha Google Chrome (vingine vina
hatihati ya kukwama kuliwezesha hili) 

* Fungua Simu janja yako na ingia katika WhatsApp. Ukiwa kule nenda
eneo la ‘Settings’ na kisha chagua WhatsApp Web kisha skani kodi ya
QR katika kivinjari cha kompyuta yako kwa kutumia simu janja yako.
Kwa kufanya hivi unaweza ukatumia WhatsApp katika kompyuta yako 

* Ukiwa unatumia WhatsApp katika Mtandao wa kompyuta (web) fungua
‘Group’ ambalo unataka kujitoa na kulifunga. Anza kuandika emoji
nyingi kadri uwezavyo ili zifike takribani 3000 katika ule uwanja wa
meseji. Kwa njia rahisi ili kulifanikisha hili inakubidi uwe una kopi na kupesti taaratibu.
kujitoa kwenye group la WhatsApp Emoji Takribani 3000
 
  * Ukishapata emoji zako takribani 3000 – 4000 (utajua tuu kwani meseji
yako itakua ni ndefu sana) bofya ‘Enter’ ili kutuma meseji hiyo. Na
hapa usiwe na haraka sana subiria mpaka Chrome iweze kutuma meseji
hiyo na subiri mpaka meseji hiyo ipate tiki moja ikiwa na maana
kwamba umetoka(imetumwa). 

* Baada ya kufanya hivyo sasa unaweza ukafunga WhatsApp Web yako na
ukienda katika WhatsApp kwa kutumia simu janja yako, wewe pamoja na
watumiaji wengine wa hilo ‘Group’ watapata meseji ifuatayo
*“WhatsApp isn’t responding”*
Ujumbe Ukisema 'WhatsApp Isn't Responding' Katika Simu Ya Android
Ujumbe Ukisema ‘WhatsApp Isn’t Responding’



Baada ya hapo hilo ‘Group’ la WhatsApp halitawezwa kutumika hata kwa mtu
mmoja kati ya wale ambao walikuwa katika ‘Group’ hilo. Hapa kila mtu
atalazimishwa kujitoa katika ‘Group’ hilo. Na kizuri ni kwamba
hawaatamjua mchawi ni nani kwani kutakuwa hakuna ushahidi juu ya jambo
hili. Wengi watajua ya kuwa labda ni matatizo ya kiufundi kutoka kwa
mtandao wa WhatsApp wenyewe.
Pia kuna uwezekano ‘Group’ kuweza kufanya kazi endapo njia hii itafanywa
kwa kutumia simu janja za iOs kama vile iPhone. Kwa Android zoezi hili
litakamilika mara moja tuu
Lingine la muhimu ni kwamba njia hii sio ya kutumia kwa *mzaha*. Maana
wengine wanaweza wakachukulia kama kamchezo flani. *Kabla ya kuifanya
fikiria kwanza*