9.4.16

FAHAMU MAMBO MUHIMU (3) KAMA UNATUMIA iPAD

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.Pengine tunatumia iPad zetu kila siku lakini kuna baadhi ya vipengele vimefichwa ndani ya vifaa hivyo na ni wachache sana wanavijua. Njia hizi unaweza shangaa zinawafanya wale wanaotumia iPad hizo kawaida tuu na kuwa watumiaji mashuhuri
Kanzia leo na wewe una uwezo wa kuwa mtumiaji uliyebobea kwa kutumia
msaada huu. Kwa kutumia njia hizi utaweza kuongeza kasi ya iPad yako.
                



*Kwa Haraka Haraka Tuufahamu Ujanja Huo* 

1. *KAMUSI KATIKA iPAD YAKO*
Kama bado hujui ni kwamba kwa kutumia iPad yako unaweza ukapata msaada juu ya maana ya maneno Fulani ambayo ni magumu kwako. Inafanya hivi kirahisi tuu kwa kukujulisha maana ya maneno magumu katika iPad kwa kutumia kamusi iliyopo ndani kwa ndani. Kama unataka kujua maana ya neno Fulani basi inakubidi kulishikilia neno hilo bila kuliachia kwa kidole.Baada ya sekunde kadhaa za kutoaliachia neno hilo yatatokea machaguo kadhaa hapo utabofya neno “define” kwa kufanya hivyo utapata kujua maana ya neno hilo. Kama maana ya neno umeipata lakini ulikua unataka toleo lingine la kamusi unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza sehemu ya ‘Manage’ baada ya maana tuu kutokea. Unaweza ukachagua moja kati ya kamusi 19 zilizopo na kisha bonyeza kialama cha mawingu kulia kwa kamusi unayoitaka ili ianze kushuka (download)

2. *WEKA iPAD YAKO MBALI NA WATOTO/WAPEKUZI*
Hapo haimaanishi inabidi uifiche, kuna njia spesheli ya kufanya hili. Kama una watu wanaopenda kupekua iPad yako kama vile kwa lengo la kucheza magemu mabalimbali (iPad ina kioo kikubwa, inatamanisha kucheza magemu mule) na cha kushangaza unaweza kuta baada ya kucheza michezo hiyo wanajikuta wanaingia katika sehemu nyingine katika iPad yako. Kuna njia spesheli ambayo inapatikana pia hata katika iPhone. Njia hii inahusisha kutoruhusu kutumia baadhi ya eneo katika skrini ya iPad au iPhone yako. Njia hii inatwa ‘Guided Access’ na sio kitu kipya lakini watu wengi hawafamu kama njia hii ipo au ni kazi gani inaweza ikafanya.
 Ili kuiwezesha nenda katika *Settings>>General>>Accessibility* na kisha washa ‘Guided Access’. Baada ya hapo itakubidi uweka neno siri kabla hujaanza itumia ili baadae uweze kukubali mabadiliko uliyoyafanya katika eneo la ‘Guided Acces’. Kila kitu kikishafanikiwa fungua App moja ambayo unataka itumiwe na kisha bonyeza kitufe cha numbani (home) mara tatu mfululizo. Ukifanya hivi kipengele cha ‘Guided Access’ kitatokea
Sasa unaweza ukachora kiboksi katika eneo hutaki litumike. Kwa mfano unaweza ukachora kiboksi hicho katika kile kialama cha kurudi nyuma (mtu hataweza kurudi nyuma, atabaki hapohapo) au kwenye eneo lolote ambalo hutaki walitumie katika skrini. Ukishamaliza kuzingushia kiboksi maeneo yote ambayo hutaki yatumiwe na watu wengine hapo unaweza ukabofya ‘Start’ kiasa ‘Guided Access’ itapotea. Baada ya hapo mtu anaweza tumia App lakini hataweza gusa yale maeneo ambayo utakuwa umeyazuia.


3. *FANYA iPAD YAKO IWE NYEPESI KIUFANISI*
Nji hizi zitaifanya iPad yako iwe nyepesi katika ufanisi maana muda mwingine inakuwa ni nzito. Kwa mfano utakuta inachelewa kufungua App nyingine wakatiki ukiwa hujafunga App zingine kadhaa ambazo ulikua umezifungua toka mwanzo. Pia iPad kwa kawaida huwa zinapunguza kazi ya ufanisi baada ya miezi kadhaa tuu, ili kuhakikisha unalikomesha hili kuna njia rahisi rahisi za kuhakikisha hili linakupita. Njia ya kwanza kabisa ni kwenda katika ‘System’ ya iPad yako na kuangalia kama ina toleo jipya la programu endeshaji. Kumbuka App na baadhi ya programu katika iPad yako huwa zinapta matoleo mapya mara kwa mara ili kuweza kuendana na matoleo mapya ya programu endeshaji. Sasa kama iPad yako inatumia programu endeshaji za zamani unaweza ukawa unalionatatizo hili la kuchelewa kufanya kazi husika katika iPad yako.
Njia nyingine ambayo huwezi kuizania ya kukusaidia kuongeza ufanisi wa ipad yako ni kufuta data za kivinjari cha Safari. Hata kama ukifungua ukurasa kupitia Safari ukawa unafunguka kwa haraka, kumbuka taarifa zinazojihifadhi katika kivinjari hicho zinaweza zikafanya iPad nzima kuwa na spidi ndogo katika utendaji.

Ili kufuta taarifa hizo nenda katika ukurasa wa *Settings>>Safari>>Clear History and Website Data*. Baada ya kufuta taarifa hizo kila kitu kilichokuwa kikihifadhiwa katika kivinjari cha Safari kama vile kumbukumbu zake na mambo mengine yatakuwa yamefutika kabisa.
Kwa kufanya hivyo utakuwa umeongeza spidi ya iPad yako hapo unaweza ukafungua App mbalimbali na kuingia katika mtandao wowote kwa kutumia kivinjari cha Safari bila ya kuwa na tatizo lolote ambalo litahusisha spidi ndogo katika ufanisi

Mpaka hapo natumai umepata maujuzi mbalimbali ambayo yatakufanya kutumia iPad pengine na iPhone yako bila ya kuwa na wasiwasi kuwa labda inaweza ikawa na spidi ndogo katika ufanisi. Kama hali hii ikitokeza baada ya muda (inaweza ikawa ni baada ya miezi kadhaa) rudia kufanya njia hizi tena.