12.2.17

Njia Rahisi (10) Za Kuongeza Followers Instagram

BY net tamaduni

Pale linapokuja swala zima la kutafuta masoko (social media marketing)
au follower kwenye mitandao ya kijamii ukweli ni kwamba ni lazima uwe
makini sana kwani usipo kuwa muangalifu utakuta unatumia hela nyingi iii
kuongeza kiwango cha mauzo kwenye biashara yako, hivyo ni vyema kuanza
na hatua fulani za kawaida au za bei nafuu (ninge pendekeza za bure) iii
kuongeza kiasi cha mauzo kwenye biashara yako hiyo mpya au hata ya
zamani baada ya hapo ndipo uwende kwenye hatua za kulipia (hapa ni baada
ya kuongeza msingi wa biashara yako hiyo).
Ni kweli kwamba kwa sasa mahali pazuri pakuanzia katika swala zima la
kutafuta masoko ni kwenye mitandao ya kijamii, Na pia vilevile tukija
kwenye swala zima la mitandao ya kijamii wote tunajua kuwa Instagram ni
moja kati ya mtandao bora sana wa kijamii kwa sasa hivyo Basi ili
kufikia hatua fulani ya mwanzo ni vyema kufuata hatua hizi ili kuongeza
follower kwenye akaunti yako mpya ya instagram au hata ambayo ilikwepo
hapo hawali, hatua hizi ni za bure kabisa na nirahisi kuzifuata.

1.Tumia Hashtags (#hashtags)

          Matumizi ya hash tags yameonekana kuongeza follower kwenye
mtandao wa instagram mpaka asilimia 50% hivyo ni vyema kutumia hashtags
pale unapokua unapost kwenye mtandao huo. Kumbuka kutumia hashtags
zinazotumiaka kwa wingi na watu mbalimbali.

2.Like Picha za Watu Mbalimbali
          Hii ni njia nyingine ambayo ukweli ni kwamba inasaidia sana,
hakikisha una like picha za watu ndani ya nchi yako ili kupata wateja
sahihi fanya kila siku angalau hata picha 50 za kwanza.

3.Tangaza Akaunti yako kwenye Mitandao mingine

          Hii ni nzuri sana kwa mtu ambaye tayari alisha anza kutafuta
masoko kwenye mitandao mingine kwani ni vyema kujulisha wateja wako kuwa
sasa unayo akaunti kwenye mtandao wa instagram.

4.Komenti Kwenye Picha Mbalimbali za Watu
          Hii ni njia ya kawaida ya kupata follower kwenye mtandao huu
wa instagram. kumbuka kukoment kwenye picha za watu ambao unahitaji wawe
wateja wako, unaweza kutafuta akaunti ya mtu anaefanya biashara kama
yako kisha kwa makini elezea baadhi ya bidhaa anazopost mwezako bila
kukashfu.

5.Post Kuanzia Saa 1pm (Mchana) Mpaka Saa 5pm (Jioni) Siku za Wiki
          Saa saba ni mda mzuri wa kupost kwani mida hii watu wengi huwa
ndio mida ya chakula cha mchana au hata wengine huwa ndio wamemaliza
kupata chakula hivyo kupata muda wa kuangalia simu zao kabla ya kurudi
kwenye majukumu ya siku. Kuanzia saa kumi na moja na kuendelea unaweza
kuendela kupromot post yako kwa kushare kwenye mitandao mingine
(facebook) magroup mbalimbali na akaunti za marafiki zako.

6.Kumbuka Ubora unazidi Wingi (quality beats quantity)
          Hapa ninamaana kuwa ni bora kupost picha nzuri na zenye msaada
kwa wateja wako kuliko kupost picha nyingi lakini ambazo hazina msaada
wowote kwa wateja na watumiaji wa bidhaa zako. Pia unawea kupost hata
post zenye kufurahisha ili kubadilisha mood za wateja wako wakati kwa
wakati (Hakikisha unapost kitu chenye kufurahisha kweli au kama ni Pole,
Shukurani au hata kingine chochote kumbuka to kumaanisha unachokipost).

7.Hakikisha Bio (Biography) Yako Imekamilika
          Ukitaka watu wakuone muaminifu nibora kujiweka kwenye
mazingira ya uaminifu, hii pia inakuwa kwenye profile yako ya instagram
kama unataka follower ambao kweli wanaweza kuwa wateja wa bidhaa yako
hiyo ni vyema uwaweke wazi unachokifanya na njia rahisi ya kufanya hivi
ni kwakutumia bio ya Profile yako kwani hii ndio njia ya inayoelezea
kitu unachokifanya na pia namna ya kukupata kwa urahisi kwa kutumia
Email, Namba za simu au hata pia kwa kutumia tovuti yako ambapo utaweza
kuwapa wateja wako maelezo zaidi kuhusu bidhaa yako.

8.Uliza Maswali Kwenye Picha ya Post (Caption) Zako
          Nivyema kuruhusu wateja wako kujadili kwa kujibu maswali
mbalimbali ambayo unawauliza kwenye post zako mbalimbali, kumbuka to
kupost vitu vya msingi kama ilivyosema kwenye hatua namba (6) sita.

9.Pendelea Kupost kwa Wingi Siku za Jumapili
          Jumapili ni siku ambazo mara nyingi watu wengi wanakua na
nafasi kubwa ya kuingia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hivyo ni
vyema sana kutumia wakati huu kwa kutafuta masoko kwenye mitandao nhiyo
mbalimbali ikiwemo instagram.

10.Elewa Wateja Wako au Watu unao Taka Wakufollow
         Kwenye swala la kutafuta masoko hakuna kitu muhimu kama kujua
mtumiaji wa bidhaa yako ni nani, maana yake ni kwamba ni vyema kujua
kuwa unataka watu wa aina gani wakufollow kwa kutafuta kwenye akaunti
mbalimbali za watu wanaofanya biashara kama yakwako utaona baadhi ya
watu ambao wanapenda bidhaa hizo hivyo wafollow nao wata kufollow back.