Karibu Net TAMADUNI.Kama wengi tulivyo na ufahamu kuwa kuna tovuti nyingi kwenye intaneti ambazo unaweza kupakua subtitles bure. Mara baada ya kupakua nakala ya subtitle unaweza kuihamishia kwenye folder la filamu husika na programu
nyingi zinazotumika kucheza video zinaweza kupakia nakala hiyo moja moja
kwenye filamu husika. Lakini unaonaje kama VLC ikapakua nyakala za
subtitles moja kwa moja kwa ajili yako?
Hatua ya kwanzanyingi zinazotumika kucheza video zinaweza kupakia nakala hiyo moja moja
kwenye filamu husika. Lakini unaonaje kama VLC ikapakua nyakala za
subtitles moja kwa moja kwa ajili yako?
Hatua ya kwanza pakua na *sakinisha(install)* toleo jipya la programu
ya VLC Media Player <http://www.videolan.org/vlc/index.html> kwenye tovuti tovuti yao rasmi.
Hatua ya pili
1. Baada ya kusanikisha toleo jipya la VLC Media Player fungua filamu
unayotaka kuitazama kisha nenda kwenye kichupo(tab) cha ‘*View*‘
2. na Bonyeza kitufe cha ‘Download Subtitles'
Hatua ya tatu
1. Katika dirisha la VLsub lililofunguka andika jina la filamu na
bonyeza ‘*Search by name*‘ na orodha ya nakala za subtitles zilizopo
itatokea.
2. Chagua nakala ya subtitle uitakayo katika orodha kisha bonyeza
kitufe cha ‘*Download Selection*‘ baada ya sekunde kadhaa nakala ya
subtitle itapakuliwa na kupakiwa ndani ya filamu.
Hii ni moja ya njia nyepesi na rahisi ya kupakua subtitles kutokakwenye intaneti kwa haraka zaidi.