Google Play Store ndio sehemu pekee ambayo watumiaji wa simu za Android wanaweza kupakua na kuinstall applications tofauti tofauti. Kuna muda inatokea unaifuta play store kwa bahati mbaya au play store iliyokuwa kwenye simu yako inapata matatizo kama kuliwa na virusi na kulazimika kuiuninstall.
Kila siku Google wanatoa updates za kuisalama na kiutendaji katika applications zao hasa Play Store ambayo ni application mama. Kwa sasa playstore ipo version (toleo namba) 6.9.15.
Hapa kuna changamoto kidogo kwani namba za matoleo ya Play Store siku zote huwa zinachanganya sana. Kuna muda Google huwa hawatoi matoleo ya playstore hadharani na kuamua kuongeza vitu bila ya watumiaji kujua. Toleo la sasa la Play Store lina uwezo kumfanya mtumiaji kujaribu (kutest) app kabla hata ya kuidownload.
Njia za kufuata;
- Fungua sehemu ya settings katika simu yako, nenda mpaka kwenye security, alafu nenda mpaka kwenye unknown sources, tiki hapo ili kuruhusu simu kuinstall apps sehemu tofauti na playstore. Kumbuka kuizima hii mara baada ya zoezi zima kwa sababu za kiusalama zaidi.
- Kwa kutumia kivinjari cha simu yako fungua XDA Developers forum or APK Mirror ili kupakua toleo la sasa la Playstore.
- Baada ya kufanya hivyo unaruhusiwa kuinstall faili la apk ulilopakua.
- Kumbuka kuzima install application from unknown sources option.