28.7.15

JINSI YA KUTENGENEZA PASSWORD NZURI NA SALAMA.

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI: Mara nyingi watu wamekuwa wakiibiwa account zao za mitandao kutokana na kutumia password isiyokuwa na protection ya kutosha. Wengi hudhani kuna ni ujuzi wa aliyeiba password ndio umesababisha hilo lakini honestly, ni wewe mwenyewe.Katika dunia hii, ukiachana na Tanzania, Internet security imekuwa ni jambo ambalo wegi huwa hawalipi kipaumbele na huishia kutengeneza password ambayo ‘ataikumbuka kirahisi’. Ok so may be utaandika labda "elibarick" au “walinazi” kwa sehemu unayoishi au chakula ukipendacho.
But, does that mean hii password haiwezi kuwa nzuri zaidi? Mambo ya kuzingatia utengenezapo password ni haya:


Bonyeza soma zaidi


1. UREFU WA PASSWORD YENYEWE
Password nzuri inabidi ianzie herufi 8 kuendelea. Kadri password yako inavyozidi kuwa ndefu ndio kidogo strength inaongezeka na inamuwia vigumu mtu mwingine kuotea. Maneno mafupi kama “matairi” au “given” si salama kutumia kama password, be creative! 


  2. USITUMIE MANENO YALIYOZOELEKA
KAMWE! Epuka kabisa kutumia maneno yaliyozoeleka. Sio tu kwa sababu mtu anaweza kuotea kwa urahisi ila kwa sababu pengine sio mtu anayeotea, pengine ni computer. Kuna kitu fulani tunakiita “Dictionary Attack“, hii ni tool ambayo hujaribu KILA NENO lililopo kwenye dictionary kwenye sehemu ya password.
So kwa mfano username yako ni “givenality”(ambayo inaonekana na kila mtu, obviously), mtu ataenda kwenye login na kuandika kwenye sehemu ya username “givenality” na kwenye sehemu ya password atafungulia hiyo tool ambayo itajaribu kila neno kwenye dictionary. Unaona ninachomaanisha eeh?
Na ndio maana nashauri kamwe usitumie neno lililo sahihi gramatically (kosea hata spelling kwa makusudi!). Personally nimeiboresha hii tool na inajaribu mpaka maneno ya kiswahili na aina za vyakula, mboga, etc (hehehe!) 


HIZI NI BAADHI YA PASSWORD ZINAZOTUMIKA SANA KWENYE INTERNET:


password
123456
12345678
1234
qwerty
12345
facebook
tanzania
112233
football
ufunguo
abcd
696969
abc123
(jina la kwanza)
(jina la pili)
master
jennifer
111111
jordan
superman
1234567 

       3. USIIHUSISHE PASSWORD YAKO NA WEWE
Ni jambo ya kawaida kwa watanzania wengi kutumia password either majina ya watoto wao, mwaka wa kuzaliwa, mke/mume/ au majina yake mawili. Si salama. Kwanini? Ni kwa sababu yule jirani yako akitaka kuingia kwenye account yako password za kwanza atakazojaribu ni hizo.
Baada ya kuzingatia hivyo, twende sasa kwenye mbinu za kutengeneza password nzuri. 


I: NJIA NDEFU NA NZURI ZAIDI
1. Tunga mpangilio wa maneno/sentensi, kisha cheza nao Fikiria kuhusu sentensi unayoweza kuikumbuka kirahisi (relax, hatutatumia sentensi yote). Kwa mfano:
“Katika watanzania ambao hawajawahi kupanda ndege mimi nimo”
Ukishapata sentensi kama hiyo chukua herufi ya kwanza ya kila neno kwenye sentensi. Hivyo:
“kwahkdmn”
Sasa hivi imeanza kuwa nzuri na inayokumbukika, na ina herufi 8! 


       2. ONGEZA NA NAMBA KUIBORESHA
Password yetu “kwahkdnm” ni nzuri, na kufikia hapo, Dictionary-attack haiwezi kuipata (wala yangu niliyoboresha haiwezi pia!) ila tunaweza kuboresha zaidi na namba. Unaweza kuweka namba labda mwanzoni, mwishoni, au hata katikati. Mfano;
“1kwah2kdmn3”
Password ni ile ile ila nimeongeza namba 123 mwanzoni, katikati, na mwishoni. Nimeanza na namba, nikaandika herufi 4, nikaweka namba tena, kisha nikaandika herufi zilizobaki, na nikamalizia na namba tena! Kuna ambaye anaweza kuotea hiyo? Ukiachilia namba 123, unaweza weka mwaka wa kuzaliwa au namba mgongoni za wachezaji wa simba/yanga unaowapenda, baadhi ya tarakimu kwenye namba yako ya simu, n.k. 


          3. WEKA ALAMA NYINGINE ZA ZIADA
Kama umeridhika kufikia hatua ya pili, ni sawa pia. Lakini kama unataka yenye nguvu, tuendelee. Sasa, unaweza weka zile alama zitumiwazo mara chache sana. Labda kama asilimia (%) au kiulizo (?) au dola ($). Mimi nitatumia mshangao (!). Hivyo basi;
“1kwah2!kdmn3”
Notice nimeweka alama ya mshangao katikati baada ya namba “2″.
Imetulia. Unaweza kuendelea? Twende!

4. HERUFI KUBWA NA NDOGO
Hii ndio hatua ya mwisho itakayopendezesha password. Changanya herufi kubwa na ndogo. Unaweza kuamua haerufi ya kwanza na ya mwisho ziwe kubwa. Mfano;
“1Kwah2!kdmN3”
Kuna mtu dunia hii anaweza kuotea password hiyo?
Sasa password yetu imekamilika!! 


II NJIA FUPI, SALAMA PIA.
Kama wewe huwezi kukumbuka password ya namna hiyo basi tumia njia hii ambayo ni salama pia, lakini sio kama ya kwanza kwa sababu hauna tarakimu:
1.Tafuta Maneno Mawili Mafupi
Kama hatua za juu ni ngumu au huwezi kumudu kukumbuka namna hizo, tafuta maneno mawili mafupi au moja refu. Mfano:
“majani”, “mabichi”
Kisha yaunganishe hayo maneno, hence:
“majanimabichi”
2. Replace baadhi ya herufi na namba

Chukua password yako, (in our case, “majanimabichi”) then katika baadhi ya herufi badilishana na namba. Mfano:-
“m4j4n1m4b1ch1“
Hapo juu herufi zote za “a” nimezibadilisha na namba “4″ (huwa nachukulia A na 4 zinafanana, so haitakuwa kazi kukumbuka). Pia i nimeibadilisha na 1. Password imekamilika! Unaweza ukawa mjanja na kuchanganya herufi kubwa na ndogo ili iwe ngumu zaidi.
Kwa mimi ningeshauri utumie njia ya kwanza kwa sababu ndio nzuri zaidi. Itaichukua computer muda mrefu zaidi kubashiri password iliyotengenezwa kwa njia ya kwanza kuliko ya pili. 
Ahsante endelea kutembelea Net TAMADUNI.