Kuna muda unajikuta upo busy na mihangaiko ya kimaisha na mmoja kati
ya jamaa zako anaamua kukutumia sms Whatsapp, kwa haraka unaiangalia ile
sms alafu unaiweka simu mfukoni ukisema nitaisoma baadae. Vitiki viwili vya bluu katika Whatsapp vinavyoashiria
ujumbe umesomwa vina faida na hasara zake hasa linapokuja suala la kazi
au mapenzi.
Chukulia kama aliyekutumia ujumbe huo ni mama mkwe, au baba mwenye nyumba yako, au bosi wako ama mpenzi wako. Hapo utaona kuna umuhimu wa kuweza kuzima hizi alama za blue zinazoonyesha kusomwa kwa ujumbe.
Tayari tulishaelekezana hapa jinsi ya kuzima last seen, read receipt na kutoa profile picha katika makala iliyopita.
Leo ngoja tuangalie njia ya haraka tu ya kukuwezesha kusoma message za whatsapp bila mtumaji kujua kuwa umeshazisoma.
- Pale message ya Whatsapp inapoingia usiifungue kwanza, nenda kwenye settings kisha weka airplane mode on, au bonyeza kitufe cha power moja kwa moja ili kupata menyu ya kuzima data kabisa
- Ni muhimu kuzima data au kuweka simu katika airplane mode ili isiwe na uwezo wa kutuma na kupokea data kwa wakati huo. Hii ni kuzuia ujumbe wa kusomwa kwa mesage usirudi kwa mtumaji na kumwonyesha tiki mbili za bluu kwa sababu data ndio inayosafirisha ujumbe huu.
- Baada ya hapo fungua application yako ya whatsapp na soma jumbe zako kwa amani.
- Ukimaliza kusoma hakikisha unazima application ya Whatsapp kabisa kwa kutumia application manager yoyote uliyokuwa nayo, kisha washa data au zima airplane mode na mtu aliyekutumia atashindwa kuona zile tiki za bluu.