27.3.18

James Goodfellow, mgunduzi wa ATM aliyelipwa $15 (Sh.32,800/=) kwa ugunduzi wake

BY net tamaduni

Kama wewe ni mtumiaji wa ATM usisahau kutoa shukrani zako za dhati kwa mgunduzi wa mashine hizo za kutolea pesa duniani kila unapoenda kutoa pesa mwaka huu.



Bwana Mark Zuckrberg ambaye ni mgunduzi wa Facebook anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilion 50, kwa ugunduzi tu wa mtandao wa kijamii unaotumika zaidi duniani kwa sasa. Hali ipo tofauti wa mgunduzi wa mashine za kutolea fedha bwana James Goodfellow, ambaye alilipwa kiasi cha dola 15 tu sawa na shilingi 32,000 za kitanzania kwa ugunduzi wake.

Katika miaka ya 1960, Goodfellow alikuwa akifanya kazi kama muhandisi katika mashirika ya Glasgow, ikiwa ni sehemu ya kiwanda cha Smiths alipewa kazi maalumu ya kusadia wateja wanaochelewa benki siku za wikiendi hasa pale benki zinapofungwa. Kwa mujibu wa Goodfellow watu wengi walikuwa wakikosa huduma za kibenki kwa sababu walikuwa wakikosa muda siku za katikati ya juma na siku za wikiendi benki zilikuwa zikifungwa mapema.

Baada ya kufikiria kwa makini akaona mashine ndio suluhisho la tatizo hili, akaja na mashine ya kutoa pesa ikihusisha PIN (Personal Identification Number) kama utambulisho wa muhusika wa akaunti. Serikali ya Uingereza ikampa hati miliki ya kuwa mgunduzi wa PIN.

Goodfellow alitengeneza kadi ya plastiki yenye matundu ambayo ilikuwa ikipachikwa kwenye mashine ya kutoa fedha kabla ya mtumiaji kutakiwa kuingiza tarakimu 10 zikiwa pamoja na PIN zake ili kuweza kutoa fedha, kwa sasa zinafahamika kama ATM cards.