2.2.17

77% ya huduma zote za kimtandao zinatolewa na Google zina usalama (Encrypted)

BY net tamaduni

Kadri siku zinavyoenda hali ya kiusalama mtandaoni inazidi kupungua, usalama wa taarifa binafsi za mtu pamoja na tovuti anazopenda kutembelea upo mashakani kwa kiasi kikubwa kutokana na matukio mengi ya kidukuzi yanayoripotiwa kila kukicha.data-encryption-google


Google wametoa taarifa na kutaja 77% ya huduma wanazotoa kwa sasa mtandaoni kuanzia huduma ya kutafuta vitu (Search Engine) na huduma nyingine zina usalama wa kutosha kwa kuwa zipo encrypted.
Encryption ni nini hasa?
Hili ni neno la kitaalamu linalomaanisha kuficha vitu vinavyotumwa kutoka sehemu moja mpaka nyingine (unaweza ukanisahihisha kwenye maoni). Mfano, unataka kutuma ujumbe kwa mnyongaji na unayempa kifurushi cha ujumbe ni mtuhumiwa anayetakiwa kunyongwa, hapa lazima utafute mbinu ili mtuhumiwa asijue kama ule ujumbe unamhusu yeye au mtu mwingine asiweze kuusoma ule ujumbe isipokuwa mnyongaji pekee.
Sasa katika encryption kunakuwa na vitu vikuu vitatu:

  1. Mtumaji wa ujumbe
  2. Funguo za kuufunga ujumbe
  3. Msomaji wa ujumbe
Mtumaji wa ujumbe lazima aufunge ujumbe kwa kutumia funguo walioamua yeye na mpokeaji, kwa mfano wanaweza wakaamua herufi A iwakilishwe na namba 5, herufi Y iwakilishwe na namba 9 na herufi G iwakilishwe na namba 3, hivyo kama neno linalotumwa ni ANYONGWE baada ya kulifunga na funguo (encrypt) litakuwa 3N9ON3WE. Hapo inakuwa sio rahisi kwa mtu asiyehusika kufahamu nini hasa maana ya ujumbe ule.
Kwa hiyo hapa ufunguo wetu utakuwa,  A=5, Y=9 na G=3 kwa mtumaji kwa mpokeaji atabadilisha mwenendo wa huu funguo hiyo kwa 5=A,9=Y na 3=G ili kuweza kuusoma ujumbe huo kirahisi.
Usihofu kama ujaelewa katika makala inayofuata nitakuelekeza aina tofauti za encryption, turudi katika mada yetu.
Vitu vyote vinavyoandikwa katika mtandao wa kutafuta wa google, barua pepe zote huwa zinakuwa encrypted kasoro huduma ya Youtube. Katika ripoti hiyo iliachiwa mapema Jumanne wiki hii google wamesema mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu 2016, watakuwa wameshakamilisha zoezi la kuencrypt mtandao wa youtube wenye watumiaji zaidi ya bilioni 1 duniani kote.
Hatua ya Google kuencrypt taarifa zote na link zote ilikuja mara baada ya Edward Snowden jasusi wa kimarekani anayeishi kwa hifadhi ya kisiasa nchi Urusi kutoa taarifa za kidukuzi zilizokuwa zikifanywa na serikali yake mwaka 2013. Snowden alibainisha serikali yake ilikuwa ikikagua taarifa binafsi za watumiaji wa mtandao bila ruhusa zao na kutaja jambo hilo kama ni ukiukwaji wa haki za usiri wa mtu.