Karibu Net TAMADUNI.Hivi karibuni zilisambaa taarifa kwamba simu feki zote nchini
Tanzania zitazimwa ifikapo mwezi Juni mwaka 2016, makala hii
itakuonesha jinsi ya kuangalia kama simu yako ni feki ama la.
Hatukuweza kuthibisha moja kwa moja kwamba kweli simu zitazimwa
mwezi Juni lakini tumejiridhisha kuwa kutakuwa na hatua dhidi ya
wanaomiliki simu feki pindi itakapofika tarehe hiyo.
Zifuatazo ni hatua unazoweza kuzitumia kuangalia kama simu yako ni fake,
hakuna mahitaji makubwa kufanya hili ila tu unahitaji simu yako
unayoitumia na unayotaka kuiangalia.
*Jinsi ya angalia IMEI namba*
* Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha kupiga
* Baada ya hapo simu yako itakuletea IMEI namba ambapo kama simu yako
au kifaa chako kina laini mbili basi kutakuwa na IMEI namba mbili
* Namba hii pia unaweza kuipata katika boksi la simu ama nyuma ya ya
simu hiyo baada ya kutoa betri, utaijua kwa kuwa huwa ni tarakimu 15.
* Nakili namba hizo pembeni.
Mfano wa IMEI namba iliyopatikana kwa kupiga *#06#
*Jinsi ya kuangalia kifaa kama ni feki ama halali*
* Iandike ile namba uliyo nakili katika hatua iliyopita katika sehemu
ya kuandikia ujumbe (SMS)
* Utume ujumbe huo kwenda namba 15090
* Baada ya kutuma meseji hiyo utaangaliziwa je hiyo IMEI namba ni ya
simu ya aina gani na nani mtengenezaji wa simu hiyo.
* Subiri majibu (haitachukua muda mrefu)
* Ujumbe huo ukija unakuwa na maelezo ya kampuni iliyotengeneza simu
hiyo pamoja na jina la simu hiyo.
jinsi ya kuaangalia simu kama feki
Mfano wa ujumbe unarudishwa baada ya kutuma IMEI namba
*Jinsi ya kujua kama simu yako ni feki*
Kama jina la mtengenezaji wa simu yako pamoja na aina ya simu yako
(Uliyo jibiwa baada ya kutuma IMEI namba) haviendani na majina ya simu
yako (ambayo yameandikwa katika simu yako) basi ujue simu yako
inamashaka na ni vyema kumuuliza muuzaji wako juu ya hilo.
Kama majina yaliyorudi hayaendani na majina yaliyoandikwa katika simu
yako basi upo katika kundi lenye uwezekano wa kuwa na matatizo,
TUNAKUSHAURI ufuate utaratibu na kuibadilisha ama kuacha kuitumia simu
hiyo kabla ya mwezi Juni.
*Kwanini TCRA wanataka tubadilishe simu*
/Simu isiyo na IMEI ni sawa na gari lisilo na namba za usajili
{plate number}/
Vyombo vya usalama vinaweza kukamata wahalifu wa kutumia mitandao ya
simu kwa msaada wa IMEI namba hivyo mtu akiwa anatumia simu ambayo haina
au ina IMEI namba ambayo sio sahihi anazuia utendaji kazi wa taasisi za
usalama hivyo wao kama mamlaka wanatakiwa kuhakikisha kila mtu anatumia
simu yenye IMEI namba sahihi.