Karibu Net TAMADUNI.Katika miaka 40 ya Apple yapo matukio mengi na mambo mengi ambayo yamefanyika lakini sio yote yanajulikana zaidi, makala hii itakuletea mambo ambayo hayajulikani saana kuhusu apple.
*1.Mjue Ronald Wayne ambaye ni mmoja ya waanzilishi wa kampuni ya
Apple.*
Ronald aliuza share zake za apple kwa dola za kimarekani 800 mda mfupi
tu baada ya yeye na wenzie kuanzisha kampuni ya Apple, inasemekana
kwamba alifanya hivyo baada ya kuhofia kwamba iwapo Apple wangeshindwa
kibiashara basi mali zake zingebinafsishwa.
Wasichojua wengi kuhusu Ronald Wayne ni kwamba anajihusisha na mahusiano
ya watu wa jinsia moja, na alimwambia habari hii Steve jobs wakati bado
wakiwa waajiriwa kabla hawajaaanzisha kampuni ya Apple.
Ronald anasema hajutii kuuza hisa zake Apple wiki chache baada ya
kuanzishwa, anadai kwamba aliyafanya maamuzi hayo kwa kutegemea taarifa
aliyokuwa nayo kipindi kile . Yeye ndiye mbunifu wa logo ya kwanza
kabisa ya Apple.
*2. Steve Jobs aliuza gari lake ili aweze kutengeneza kompyuta ya
kwanza ya Apple*
Pesa ambazo ziligharamia utengenezwaji wa Kompyuta ya kwanza ya Apple
ambayo ilikuwa inajulikana kama */Apple computer 1/* ama */Apple 1/*
zilitokana na pesa zilizokusanywa baada ya Steve Jobs kuuza usafiri wake
wa pekee wa */VW mini bus/* na Steve Wozniak kuuza calculator yake ya
/*HP-65*/
Jobs aliuza usafiri wa pekee ili kulipa gharama za kutengeneza kompyuta
ya kwanza, gari hilo lilikua kama hili.
*3. Kompyuta ya kwanza ya Apple ilichukua siku kumi tu*
Baada ya kuwa na pesa kwa ajiri ya kutengeneza kompyuta iliwachukua
/Apple/ siku kumi kukamilisha kazi. Kompyuta hiyo ikauzwa kwa dola za
kimarekani */666.66/* Wozniak anasema hakuwa anajua chochote kuhusu
mambo ya kishetani kuhusishwa na namba hiyo kwa wakati huo hivyo hiyo
namba haina uhusiano wowote na imani za kishetani.
*4. Steve Jobs aliwahi kushwa cheo akaamua kwenda kuanzisha kampuni
nyingine.*
Mwaka 1985 Steve Jobs alishushwa cheo cha umeneja na bodi ya wakurugenzi
baada ya kutokea kugombea madaraka katiyake na aliyekuwa mkurugenzi
mtendaji wa wakati huo, Jobs akaondoka na baadhi ya wafanyakazi
wakaanziasha kampuni ya *NEXT.*
Hata hivyo mkurugenzi mtendaji aliyesababishwa kuondoka kwa Jobs Apple
alisababisha hisa kushuka na hivyo akaondolewa na baada ya muda
akaajiriwa mtendaji mwingine ambaye alimrudisha Jobs Apple kwa kununua
kampuni ya NEXT. Tukisheherekea miaka 40 ya Apple tujifunze kutoka kwa
mwanzilishi wake Jobs ambaye hakukata tamaa aliposhushwa cheo katika
kampuni yake.
*5. Apple walishawahi kuwa na pesa nyingi kushinda serikali ya Marekani*
Kwa kipindi kifupi mwaka 2011 Apple walikuwa wanahifadhi ya pesa kubwa
hata kushinda hifadhi ya pesa ya Serikali ya Marekani, Hii ilitokana
hasa na ukubwa wa madeni ya Marekani kwa wakati huo.
Yako mambo mengi ambayo hayajulikani kwa watu hasa watumiaji wa bidhaa
za Apple hayo matano ni ni machache ambayo mimi ninmepata kuyafahamu,
wakati tunasheherekea miaka 40 ya Apple.