7.11.15

CHEKI JINSI YA KU- CONVERT NYIMBO NA VIDEO KWA KUTUMIA VLC.

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.VLC ni programu ya bure yenye uwezo mkubwa pia wakubadilisha mafaili kutoka kwenda mfumo mmoja kwenda mfumo mwingine; mfano kutoka.AVI kwenda .MP4 au .MP3 n.k. Je ulikuwa unafahamu ya
kwamba VLC inaweza kufanya kazi hiyo pia?


Mara nyingi inaweza ikakubidi ubadilishe mfumo wa faili la wimbo
au video kutoka aina moja kwenda aina nyingine ili uweze kutumia
katika kifaa chako husika – simu, tableti n.k.



Hatua ya kwanza

Fungua programu ya VLC


Hatua ya pili
                             


Bofya eneo la *Media* -> *Convert/Save*, Kisha bofya ‘*Add*‘ na uchague
faili unalotaka kulibadilisha mfumo (covert)



Hatua ya tatu

Hapo hapo eneo la *Convert* pia linaonekana, mbele ya ‘*Profile*‘ bofya
na uchague mfumo mpya unaotaka faili hilo liwe


Hatua ya nne
Kwenye eneo la ‘*Destination*‘ kunamaanisha eneo ambalo faili jipya
litawekwa, unaweza pia kulipa jina jipya. Bofya ‘*Start*‘ na VLC itaanza
kazi ya ku’covert faili husika.

Kutegemeana na ukubwa wa faili lako basi kazi hiyo inaweza ikafanyika
ndani ya muda mfupi au dakika kadhaa. Mara nyingi video ndio zinachukua
muda mrefu.

*Ingawa VLC inauwezo wa kufanya vitu vingi ni kwamba tuu hawajitangazi
sana kwa kujipa sifa kama huduma zingine hasa zile zinazotafuta pesa
(yaani za malipo) katika kufanya haya.*