Kulinda simu yako au tablet yako ya Android hakuishii kwenye kuweka screen lock tu, la hasha kuna njia nyingine nyingi za kuifanya simu na data zako kuwa salama muda wote.
1. Weka Screenlock
Kuweka lock kwenye screen yako ni njia moja ya muhimu ya kuilinda simu yako hasa pale unapoipoteza au unapoiacha kwenye mikono isiyo salama. Katika mfumo endeshi wa android unaweza ukaweka screen lock tofauti kama PIN lock, Pattern lock, Password lock au Fingerprint scanner kama simu yako inauwezo huo. Kuna baadhi ya matoleo unaweza ukaweka voice lock au eye scanner lock. Hii inamzuia mtu mwingine asiyehusika na simu yako kuweza kuifungua bila ridhaa yako. Kuset screen lock fungua Settings–> Security–> Screen lock na hapo utachagua inayokufaa.2. Lock Application zako za msingi, picha pamoja na video
Unaweza ukaongeza ulinzi katika application zako ambazo hutaki mtu mwingine aweze kuzitumia au kuzifungua kwa kuzilock kwa kutumia baadhi ya application za kulock mafail na application kama App Lock inayopatikana googe play store. Hii itakusaidia sana kulinda taarifa zako za ndani hata kama mtu amefanikiwa kutoa screen lock yako.3. Hakikisha Mfumo Endeshi wako (OS) pamoja na Application zote unazotumia zipo Updated
Hii ni ya msingi zaidi kwani wengi wetu tumekuwa tukipuuzia kupdate application zetu hata pale zinapotuomba kuziupdate. Makampuni yanayotengeneza application husika huwa wanaziupdate sio tu kuongeza vitu vipya au kuongeza ufanisi, hapana bali kuziba mianya yote ya kiusalama iliyoachwa wazi hapo kabla. Unatakiwa kuset simu yako iwe inaupdate application zake automatically pale tu zinapotoka kwa kufungua Settings–> General –>Auto update application ( Hapa inategemea na toleo la android unalotumia).4. Usidownload Application nje ya Googleplay store
Kwa kawaida simu yako huwa haikuruhusu kudownload application nje ya play store, ila unaweza kubadilisha hili kwenye settings–> security–>Device Administration –> Unknown sources kiurahisi. Sasa sio vizuri kabisa kupakua application nje ya play store kwa usalama wa simu yako. Wadukuzi wengi wamekuwa wakitumia mwanya huu kuiba data za mwenye simu au hata kuiharibu simu yenyewe (Kwa wenye tecno Y6 na H6 watakuwa mashuhuda wa simu zao inafikia kipindi huwezi kuicontrol) . Kwa hiyo unatakiwa kuzima hiyo kama unajua unachokifanya na unauhakika na application unayotaka kuinstal.5. Kuwa makini na Application Permissions wakati unapoziinstal
Hii ni ya muhimu na kuzingatia sana, mara nyingi huwa tunapoinstal application kutoka Google Play huwa zinaomba ruhusa ya kutumia baadhi ya vitu katika simu yako. Kwa mfano punde tu unapoanza kuinstall Whatsapp huwa inaomba ruhusa ya kusoma majina na namba za simu zako, kutumia kamera yako pamoja na kutumia kinasa sauti chako, mara nyingi huwa tunaziruhusu kwa kubonyeza allow. Sasa hapa ni kwa kuzingatia zaidi hasa unapojaribu kuinstal application ambazo zinaomba ruhusa ya kutumia namba zako za simu au picha zako, lazima uwe na uhakika na hiyo application kwanza.Kwenye toleo jipya la Android Marshmallow unauwezo wa kuruhusu au kuzuia ruhusa kwa application hata kama tayari umeshainstall.