17.9.15

Kwa watumiaji wa Facebook, tegemea mabadiliko haya wakati wowote.

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI: Facebook ndio mtandao wa Kijamii ambao unatumiwa na watu wengi zaidi, Takwimu zinaonesha Duniani kuna jumla ya watu kama Bilioni 7 hivi, alafu Ripoti ya The Statistics Portal 2015 inaonesha watumiaji wa Mitandao ya Kijamii wako Bilioni 1.96, na kati yao zaidi ya 70% ni watumiaji wa mtandao wa Facebook !!


Mark Zuckerberg katupasha kuhusu mipango mingine ya Facebook, sasahivi kama ukiandika post yoyote au ukiingia kwenye ukurasa wa mtu yoyote wa Facebook unakutana na alama tatu, alama ya ‘LIKE’, ‘COMMENT’ na alama ya ‘SHARE’… lakini CEO Zuckerberg anasema ni maombi ya muda mrefu watumiaji wa Facebook wanataka iwepo na alama ya DISLIKE, yani kama kitu hujakipenda unabonyeza tu hapo.
1014_mark-zuckerberg-e1413303739290-1940x1091
Mark Zuckerberg, Boss wa Facebook.
Watu wengi wameulizia kuhusu kuwepo alama hiyo, leo ni siku maalum kwa sababu natangaza rasmi kwamba tunashughulikia hicho kitu na muda sio mrefu tutakiweka kwenye majaribioMark Zuckerberg.
Hiki hapa pia kipande cha Video kinachomwonesha Zuckerberg akiongelea umuhimu wa kuwepo button ya ‘DISLIKE kwenye Mtandao wa Facebook.