USB Debugging kama inavyosomeka katika sehemu ya settings (mipangilio) ya mfumo endeshi wa android inaonekana kama kitu kigumu sana kwa baadhi ya watumiaji wa simu za mfumo endeshi huu. Hapana, USB Debugging ni rafiki yako wa karibu na unapaswa kumtumia pale unapolazimika.
Kwa kifupi USB Debugging ni njia inayoruhusu simu yako ya android kuweza kuhamisha mafaili kati yake na kompyuta. Kwa maana ya kitaalamu zaidi, USB Debugging ni njia ya kutest (kujaribu) au kugundua bugs (mapungufu) katika application za android inayotumiw zaidi na madeveloper wa applications mbalimbali za mfumo endeshi huu.
Mara nyingi USB Debugging hutumika katika kujaribu software mbalimbali zilizotengenezwa na Android Studio, hapa madeveloper watakuwa wanaelewa zaidi. Kuinstall Custom ROM, Kuroot au hata kubadilisha baadhi ya vitu katika software.
Jinsi ya kuwasha (Enable) USB Debugging
Kufungua USB Debugging, inakupasa kufungua kuruhusu ‘Developers Options’ katika simu yako kwa sababu katika matoleo ya sasa huduma hii huwa inafichwa. Fuata hatua zifuatazo kufanya hivyo;- Fungua sehemu ya settings kwenye simu yako, shusha chini mpaka katika sehemu iliyoandikwa About Phone.
- Baada ya kufungua About Phone, shuka mpaka chini kwenye sehemu iliyondikwa ‘Build Number’, bonyeza mara saba hapo ili kufungua developers options. Baada ya kubonyeza mara saba utakuja ujumbe utakaokupa tahadhari kuwa unaelekea kufungua developers options.
- Baada ya hapo rudi nyuma kwenye menu yako ya settings na utaona Developers Options ipo katika settings, ifungue na anza kushusha chini kuitafuta USB Debugging na iruhusu.
Kwa watumiaji wa matoleo ya chini ya Android 2.3 wanaweza kufungua moja kwa moja deveopers options kwa sababu inakuwa haijafungwa na wataweza kuona hii setting ya usb debugging.