inite.com ni sehemu pekee unayoweza kudownload na
kuinstal software za Windows bure na kwa usalama zaidi kwa pamoja.
Utofauti wa ninite.com ni uwezo wa kudownload na kuinstal software
nyingi kwa wakati mmoja yenyewe bila kumsumbua mtumiaji wa Pc kuclick
Next, Next…
Tunapobadilisha Windows au tunapohamia toleo jingine la Windows
(Upgrade) huwa tunapata tabu sana katika kutafuta installer za software
zote za msingi kama Google Chrome, Adobe reader, Skype, Mozila Firefox,
VLC media player na kuziinstall mojamoja mpaka tunaporidhika. Kwa
kompyuta moja inaweza isiwe shida sana lakini ni tofauti kama una
kompyuta zaidi ya moja, kuzidownload na kubonyeza Next, next… ni jambo
la kuchosha kidogo.
Hapa ndipo ninite.com
inapoingia, ninite itakusaidia kuinstall application zote za muhimu
bila tabu wala usumbufu wowote ule. Katika mtandao (tovuti) ya ninite
utaona maelekezo jinsi kuinstal application unazotaka, hakuna kitu
kigumu zaidi ya kuchagua application au software unazotaka na kuinstall
bila tabu. Ninite yenyewe haitachagua offer au tools bars zinazokuja na
baadhi ya installer hivyo kukupa usalama zaidi.
kufahamu zaidi tembelea ninite.com