2.2.17

Ripoti zinasema matangazo ya mtandaoni kushika kasi zaidi ya matangazo ya kwenye Television

BY net tamaduni

Inasemekana mwaka 2017 kwa mara ya kwanza matangazo ya kibiashara kupitia mtandaoni yataongoza kwa mapato zaidi ya yale ya kwenye Television (runingani) kama shirika la ZenithOptimedia lilivyodai katika ripoti yake iliyotoka hapo Jumatatu.



Zenith wanasema uhitaji wa matangazo katika mtandao utaongezeka mara dufu mwaka 2017 sawa na mara tatu ya uhitaji wa matangazo wa hivi sasa kutoka na makampuni kupendelea kutangaza zaidi katika Social Media pamoja huduma za kutafuta mtandaoni (Search Engines).
Ripoti hiyo inadai desemba mwaka 2017 hali ya uchumi wa dunia itabadilika kwa matangazo mengi kuhamia katika mtandao. Wanadai hii haitawatikisa wafanyabiashara kwani biashara zao zitaendelea kukua katika kiwango kilekile sawa na walivyokuwa wakitangaza kupitia katika runinga.