Leo katika makala zetu za teknolojia tunaenda kuangalia aina hii ya kuunganisha mtandao kwa muundo wa nyavu maarufu kama mesh topology.
Hebu tuangalie baadhi ya maana za maneno kabla hatujaendelea (meaning of terminologies)
- Network – Kwa lugha rahisi ni mtandao wa vifaa vinavyoweza kuwasiliana.
- Topology – Mpangilio wa vifaa katika mtandao husika, inaweza ikiwa katika chumba au katika jengo
- Node – Kifaa chochote kilichounganishwa katika mtandao husika kama kompyuta, printer au simu na inakuwa na anuani ya kipekee (unique address) inayomwezesha kuwasiliana na vifaa vingine.
Faida za Mesh Topology
- Kila kompyuta huunganisha na kompyuta nyingine iliyopo kwenye mtandao hivo huimarisha usalama wa data inasafirishwa kati ya hizo kompyuta.
- Ni muundo wenye nguvu na hauharibiki kiurahisi kwasababu unahusisha kompyuta chache tu.
- Ni rahisi kugundua tatizo liko wapi na kutafuta nia za kutatua tofauti na miundo mingine kama Star topology, tree topology na zinginezo tutakazozungumzia wakati mwingine.
- Hutunza na kuimarisha usiri na faragha (privacy) ya data yako.
Mapungufu ya Mesh Topology
- Kuunda mtandao huu wa Mesh ni ngumu sana kwasababu unahitaji kuunganisha kila kompyuta na nyingine haijalishi ziko nyingi kiasi gani.
- Inagharimu pesa nyingi sana kwasababu huitaji cable na nyaya nyingi sana kukamilisha muundo huu.
- Inahitaji ufundi mkubwa na mtu mwenye ujuzi mkubwa sana wa maswala ya mitandao kutengeneza mesh topology.!!
Aina mbili za Mesh Topology
Japokuwa muundo wa mesh topology hautumiki mara nyingi sana kwasababu ya gharama na ugumu wake katika kuunda, zipo aina kuu mbili za mesh topology nazo ni;- Fully connected mesh topology – hii ni pale ambapo kila kompyuta inaunganishwa moja kwa moja na kompyuta nyingine ndani ya mtandao mmoja. Mfano mzuri ni hiyo picha hapo juu.
- Partially connected mesh topology – hii ni pale ambapo baadhi tu ya kompyuta katika mtandao zinaunganishwa moja kwa moja na kompyuta nyingine katika mtandao.