Kampuni ya Asus imeendelea kutoa bidhaa mpya katika mkutano wa kibiashara wa Computex unaofanyika huko Taipei kwa kuachia matoleo matatu makali ya Laptop ambayo ni Asus Transformer
3, Asus Transformer 3 Pro na ZenBook 3.
Asus Transformer 3 ni nyembamba na nyepesi sana huku
ikiwa na upana wa 6.9mm, na kioo cha 12.6 inchi na mwanga wa nits 450
na kuifanya kuwa mashine nzuri kwa matumizi ya nje. Pia ina betri yenye
uwezo wa kudumu kwa zaidi ya masaa 9 na keyboard ya kuchomoka . Asus Transformer 3Transformer 3 Pro yenyewe ni nyembamba zaidi ikiwa
na upana wa 8.35mm, kioo cha 12.6 kama Trasformer 3 na kamera ya mbele
yenye uwezo wa 13MP huku ikipewa nguvu na processor kutoka intel familia
ya Core i7 na RAM mpaka 16GB.
Asus Transformer 3 ProZenBook 3 inaonekana imekuja kwa lengo maalumu la
kupambana na MacBook kutoka Apple ikiwa na uzito wa kilo 2 tu. Inapewa
nguvu na Processor ya Intel Core i7 na betri lenye uwezo wa kukaa na
chaji mpaka masaa 9 kwa kuchajiwa mara moja.