7.2.17

Picha za Simu Mpya za Huawei P10 pamoja na P10 Plus

BY net tamaduni



Baada ya kutoka kwa Huawei P9 sasa tumesha anza kusikia tetesi kuhusu
simu mpya ya Huawei P10, simu hii inayotarajiwa kutoka mwanzoni mwa
mwaka huu ni moja kati ya simu zinazotarajiwa kuwa na ubora wa hali ya
juu pamoja na maboresho mengi.
Kwa sababu kazi yetu ni kukuletea habari zote za teknolojia basi ni
vizuri kukupa habari kuhusu tetesi hizi za picha zilizosambaa mtandaoni
siku za karibuni. Picha hizo zinaonekana kuonyesha simu inayothaniwa
kuwa ni (renders) mfano wa simu za Huawei P10 pamoja na P10 Plus zikiwa
na rangi ya nyeupe yenye gold (white-golden).

Simu hizi za Huawei P10 na P10 Plus zinategemewa kutuka kwenye mkutano
wa CES wa mwaka huu 2017. Simu hizo pia zinategemewa kuja na sifa za
simu hii inategemewa kuja na kioo cha inch 5.5, Ultrasonic fingerprint
sensor, kamera mbili za nyuma zilizotengenezwa kwa teknolojia ya leica
vyote vikiwa vinaendeshwa na processor ya Kirin 960 chip pamoja na Ram
ya GB 4 ikiwezesha simu hizo kuifadhi data kwenye memory yake ya ndani
ya GB 64 kwa Huawei P10 pamoja na GB 124 kwa Huawei P10 Plus.

Kuhusu tarehe ya kutangazwa kwa simu hii ya Huawei P10 inatarajiwa
kutoka tarehe 26 February kwenye mkutano wa Mobile World Congress
 utakao fanyika uko nchini Barcelona.