Bootloader au Recovery environment ni sehemu ya ndani ya mfumo endeshi wa android inayoweza kutumika ikiwa umesahau pattern za screen lock, kuroot simu yako au kuupgrade OS yako pale unapotaka.
Kuna muda unahitaji kufanya Factory Reset (hard reset) katika simu yako, kwa nini ufanye hard reset?
- Sababu ya kwanza inaweza ikawa kuondoa pattern au password zilizosahaulika
- Kuondoa Virus au Malware walioingia kwenye simu yako na ni ngumu kuwatoa kwa njia ya kawaida
- Kurudisha mipangilio ya kifaa chako kama ilivyokuwa hapo awali wakati kinatoka kiwandani
- Kupata eneo katika diski hifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadae
- Kuondoa taarifa zako zote kwa pamoja kabla ya kuuza kifaa chako
Kuingia kwenye bootloader sio kitu unachoweza kufanya kila siku kama kupiga simu, ni kitendo kinachofanyika pale tu unapokuwa na shida ya muhimu kufanya hivyo.
Njia za kufuata ili kuingia kwenye Bootloader;
1. Kuingia kwenye bootloader moja kwa moja kwa kutumia simu yako2. Kuingia kwenye booloader kwa kutumia PC
Kuingia kwenye bootloader moja kwa moja kwa kutumia simu yako ndio njia tutakayoizungumzia siku ya leo,
Kuingia kwenye bootloader kwa kutumia simu yako moja kwa moja, ni lazima uzime simu yako kabisa (power off your mobile device). Njia hizi zinaweza kufanya kazi kwa asilimia 99.5% kwa vifaa tajwa hapo chini, kama simu yako itashindikana usisite kuwasiliana nasi.
Google Nexus: Bonyeza kitufe cha kushusha sauti na kitufe cha power kwa wakati mmoja, pale alama ya google inapotokea achia na simu itaingia kwenye recovery mode.
Samsung: Samsung haina ‘bootloader’ kama inayotumika na simu nyingine, wao wanatumia ‘Download mode’ yenye sifa kama za bootloader. Kuingia katika Download mode, zima simu yako kabisa, bonyeza kitufe cha kushusha sauti, kitufe cha kuwashia (power button) na kitufe cha home (kitufe cha katikati kwa chini kile cha duara) mpaka logo ya samsung itakapotokea achia. Kufunga, bonyeza vitufe vyote vya sauti kwa pamoja ,home button na power kwa pamoja.
Simu za LG: Bonyeza kitufe cha kushusha sauti na power button kwa wakati mmoja mpaka pale logo ya Lg itakapoanza kutokea. Ikigoma, jaribu kuachia kidogo pale logo ya LG inapotokea alafu bonyeza tena vitufe hivyo mpaka pale itakapoingia kwenye bootloader.
HTC: Kwenye HTC bonyeza kitufe cha kushusha sauti, huku ukiwa umebonyeza kitufe hicho washa simu. Bootloader katika HTC hufahamika kama ‘Fast boot’.
Motorola: Bonyeza na shikilia kwa sekunde kadhaa kitufe cha kushusha sauti na kitufe cha power kwa pamoja.
Kwa komandi zote hizo bado bootloader inaweza ikachelewa kidogo kutokea, hivyo unashauriwa kusubiri kidogo.
Kwa simu kama Tecno, Huawei pamoja na iTel inategemea na toleo husika ila zote ni kubonyeza kitufe cha kuongeza sauti pamoja na kitufe cha power kwa wakati mmoja.
Baada ya hapo unaweza kufanya chochote unachotaka kwa kufuata maelekezo ya kwenye screen.