App hii amabayo kimsingi itakuruhusu kuchagua namba kadhaa za simu
ambazo zitapewa uwezo wa kupata location yako katika simu, unaweza
kuamua kusambaza /location/ yako ama moja kati ya namba ulizoweka kama
trusted contact inaweza kuomba taarifa za mahali ulipo na kupewa (iwapo
hautazuia ombi hilo).
App hii inaweza kutumika katika nyakati mbili kama ifuatavyo
- Ukiwa katika matatizo
Kwa mfano upo katika jengo la ofisi yenu na kuna moto umeshindwa kutoka
unaweza kusambaza /location/ yako hii itawasaidia ndugu zako kuweza
kusaidia ukaokolewa kwa haraka zaidi.
- Ukipotea mitaa
Mara nyingi tunaenda mitaa ambayo hatuifahamu vizuri na kupotea sio
jambo geni ( labda kama unapotea mtaa huo huo kila siku 😂😂😂)
ukijikuta katika mtaa umepotea na unaona noma kuonekana mshamba kwa
kuuliza basi unaweza kumtumia ramani ya ulipo mtu anayeifahamu mitaa
vizuri kisha yeye atakuelekeza.
Hii ni app kwaajiri ya kina nani hasa?
Hii app inatabiriwa kuwa itapendwa na wazazi ambao wangependa kufuatilia
nyendo za watoto wao, pia kwa wapenzi ambao kidogo wana wivu na wenza
wao ama ambao wanahisi wapenzi wao sio waaminifu ( kaeni tayari wenye
michepuko, wake kwa waume 😂😂😂)
Ili kufanya kazi vizuri app hii basi inahitaji wewe na hao watu unataka
uweunapata taarifa zao muwe mmeipakua na kuiweka app hii katika simu zenu.
Iwapo simu itazima kwa kuishiwa betri ama kukosekana mtandao ulipo basi
app hii itatuma taarifa za mahali ulipokuwepo mwisho kabla simu haijazima.