GOOGLE ADSENSE NI NINI
Ni mfumo wa Matangazo kwa njia ya mtandao unaohusisha matangazo kwenye
kurasa za tovuti , programu , blogu , majukwaa na huduma zingine za
mawasiliano haswa kwenye mtandao .
Google Adsense ina aina 2 za matangazo kuna yale ya maandishi pekee
yaani Text na yanayotembelea kama picha na video yote ni mazuri na yote
yana gharama zake .
GOOGLE ADSENSE NA MAISHA YAKO
Kwa kutumia Google Adsense unaweza kupata karibu laki 9 na zaidi kila
mwezi na ukasahau kufanya shuguli zingine , Adsense inaweza kufunga
Akaunti yako muda wowote au blogu yako muda wowote ule usipozingatia
Masharti yao , kwahiyo usitegemee sana ,
GOOGLE ADSENSE INAFANYAJE KAZI
Kama unatovuti yako ukiweka matangazo ya mfumo wa adsense utalipwa
kutokana na wingi wa watu wanaitembelea tovuti hiyo na jinsi watu
watakavyo gonga click matangazo hayo.
NOTE > Kufuatilia masharti na maelezo mengine ni muhimu sana kwa mfano
unatakiwa usiwaambie watu wagonge matangazo yako waache wa gonge click
wenyewe ukifanya hivyo unaweza kufungiwa .
SWALI MUHIMU
Je ukubwa wa Tovuti au Blogu au umaarufu ndio kuongeza kipato cha Adsense ?
Jibu ni hapana utaweza kupata mapato zaidi kutokana na jinsi ulivyoweka
matangazo yako na jinsi watu wanavyogonga matangazo hayo hapo ulipoweka
kwenye kurasa za tovuti au blogu yako
USAJILI WA GOOGLE ADSENSE UKOJE
Wale wanaotumia huduma za Gmail ambayo ni mali ya Google ni rahisi
kujisajili ili kutumia mfumo wa Adsense kwenye blogu na tovuti zao
unaweza kutembelea www.google.com/adsense www.google.com/adsense
www.google.com/adsense
NOTE>Kila mtu anahaki ya kuwa na Akaunti yake ya Adsense na kufuatilia
malipo yake mwenyewe na kulipwa yeye.
KUKUBALIWA NA PIN NUMBER
Usajili wa Goolge Adsense hauwezi kukamilika kama huna PIN NUMBER na
kujaza vitu vingine vya kuthibisha jinsi unavyolipa kodi , kama uko nchi
za ulaya kuna namba unatakiwa kuandika ndio utapewa PIN NUMBER .
Kama uki nje ya ulaya kama Tanzania , unaweza kutumiwa PIN NUMBER
kutumia DHL ambapo utaingiza namba hiyo kukamilisha mfumo wa usajili au
unaweza kuwatumia google kitambulisho au aina nyingine ya utambulisho
kuthibitisha uwepo wapo kama kadi ya benki au passport.
NOTE> Bila pin Number hutoweza kutambulika kwenye mfumo wa google
adsense na malipo yako hutopatiwa .
MALIPO YA GOOGLE ADSENSE
Google huwa inalipa wenye Adsense kwenye tovuti zao kila mwisho wa mwezi
kwa mfumo wa cheki , benki au western Union kutegemea na nchi ambayo mtu
yupo , malipo hulipwa pale kunapokuwa na kiasi cha pesa kuanzia dola 100
kwa mwezi ambapo dola 17 hutumika kama gharama za kusafirisha cheki kama
uko nchi ambayo wanatuma cheki .
Kwahiyo unavyofanya kazi hii ya matangazo hakikisha unapata hela nyingi
zaidi ili uweze kulipa gharama za benki na usafirishaji wa cheki yako ,
angalau uweze kuwa na dola za kimarekani 700 kila mwezi .
NOTE> Malipo ya kila mwezi hulipwa mwezi unaofuatia kama yalifikia
zaidi ya dola 100 za kimarekani
MALIPO YANAVYOTUMWA
Kwa nchi ya Tanzania malipo ya Google Adsene huja kwa njia ya DHL ambapo
hufika kila tarehe 2 kila mwezi , malipo yakifika kwenye ofisi za DHL
wateja hupigiwa simu na kupelekewa au kama unaweza kufuatilia mwenyewe
kutumia tracking number ya DHL kujua kama mzigo umefika au la .
Jambo la kujua ni kwamba watu wengi hufikiri cheki zinatumwa kwa njia za
posta za kawaida hapana ni DHL .
UTARATIBU WA KIBENKI
Unatakiwa uwe na Akaunti kwenye benki yoyote Tanzania kwa sababu cheki
za google huandikwa jina la mtu au kampuni kwahiyo lazima uwe na Akaunti
kama uko Tanzania .
Ukishaweka cheki kwenye Akaunti yako huchukuwa siku 21 za kazi ili
kuweza kulipwa malipo kwenye Akaunti yako na gharama zingine za kibenki .
Kutokana na gharama nyingine za kibenki ina maanisha ukiwa na shilingi
laki 5 kwa mwezi ujiandae kutoa alfu 70 kama gharama za kushugulikia
Cheki yako kwenye benki yako.
NOTE > Watu wengi hukata tamaa mapema na huishia njiani kwahiyo
wanapoteza hela zao nyingi na watu wanatangaza kwenye tovuti au blogu
hizo bure .
Kumbuka unavyofungua blogu ukaweka adsense matangazo yataendelea kuwa
hapo na watu wataona wanavyotafuta vitu mbalimbali kwenye mtandao
kwahiyo usikate tamaa mapema .
ZINGATIA NA UWE MAKINI NA MATAPELI
Hapo juu nimesema kila mtu ana haki ya kuwa na Akaunti yake ya Adsense
na kulipwa kwa jina lake hela yake mwenyewe , kuna watu wa nchi za nje
haswa Uganda wanapenda kuwalaghai watu wa Kenya na Tanzania kwamba
washirikiane kuendesha Mfumo wa Adsense kwenye tovuti zao na kugawana
Hela nusu kila mwisho wa mwezi .
Usikubali kuingia kwenye mtego huu , unatakiwa uwe na Akaunti yako
unayoweza kuitolea maelezo na inayolipwa kwa jina lako kwenye nchi yako
unaporuhusu hivyo faida haiendi nchini mwako inaenda Uganda kwa jina la
Raia wa Uganda ambaye atatumia jina bandia ili asimwone akisha kutapeli
hela zako .
Hata kama unapata hela kidogo mfano dola 1 kwa siku usikate tama utaweza
kuongeza vitu kwenye tovuti yako haswa kwa lugha ya kiingereza na
kifaransa na kuweza kupata hata dola 50 kwa siku moja jinsi
unavyoendelea kukuwa .
CHANGAMOTO ZA MFUMO HUU
Baadhi ya maeneo Adsense haifanyi kazi kutokana na aina ya matangazo
yaliyofungiwa kutokana na mila na desturi za maeneo hayo .
Mfumo wa Adsense uko zaidi kwa lugha ya kiingereza na nyingine za
kimataifa bado haijasambaa sana kwenye lugha zingine ndogo ndogo kama
Kiswahili ingawa mtu anaweza kutangaza pia
Benki nyingi haswa za afrika hazitambui mfumo wa google adsense kwahiyo
baadhi ya watu wanapata tabu pale wanapoenda kuingiza cheki zao kwenye
Akaunti na kudhani ni utapeli badala yake nyingi hutumwa kupitia
CITIBANK ambayo huduma zake ziko juu sana .
Nchi nyingi hazina mfumo wa kulipa kodi kwa njia ya mtandao kwahiyo
unakuta wanachama wote wa google adsense wanalipa kodi kwenye nchi ya
marekani kwa kwa kila malipo ya adsense nchi nyingi zinapoteza malipo
hayo kutokana na mifumo yao .
Kwa sasa nchi ya Kenya na Uganda wamefanya mazungumzo na google kwahiyo
ukiwa nchi hizo malipo yako unapata baada ya siku 3 kila mwezi kwa njia
ya western union au kuingiziwa fedha kwenye Akaunti yako moja kwa moja .