ebay ni sehemu ambayowauzaji(Seller)na wanunuaji(Buyer) wanakutana Muuzaji(Seller) anajiunga
kwa kufungua Account ebay na kisha anatangaza kitu anachokiuza akiwa
popote pale DunianiMnunuzi(Buyer)anajiunga kwa kufungua Account ebay popote alipo
Duniani kisha anachagua bidhaa nayoitaka iliyotangazwa
na Muuzaji(Seller) ana inunua online.
kwa kufungua Account ebay na kisha anatangaza kitu anachokiuza akiwa
popote pale DunianiMnunuzi(Buyer)anajiunga kwa kufungua Account ebay popote alipo
Duniani kisha anachagua bidhaa nayoitaka iliyotangazwa
na Muuzaji(Seller) ana inunua online.
Ili kukamilisha zoezi la malipo na kuuziana bila kuibiana ndio sasa
anaingia Pay pal
Pay Pal ni njia ya malipo ambapo mtu yeyote anajiunga ili mradi awe ni
mteja wa Bank inayotoa Card za Master au Visa Card
Kibongo Bongo CRDB wapo vizuri, baada ya kufungua Acc na
kupewa Master/Visa Card yako unarudi tena CRDB kuomba wai
link Master/Visa Card yako iweze kufanya online Transaction kwa kujaza
form maalumu then you're done
Baada ya kadi yako kuwa Linked unajiunga kwa kufungua Acc Pay Pal kwa
maana ya kwamba unawapa details za Account yako na kuwapa ruhusa kutoa
pesa kwenye account unapo waomba kufanya hivyo
Jinsi ebay na Pay Pal wanavyofanya kukamilisha mpango mzimaebay ni kama soko ambalo watu hawaonani, mmoja yupo Hong Kong anauza
iphone mwaingine Yupo Manzese Tz anataka kuinunua lakini wanakuta online
through ebay. so huwezi ukamtumia tu mtu hela kwenye acc ya bank maana
anaweza kuingia mitini na asiwepo wa kufuatilia
Sasa wanapotaka kulipana Pay Pal anaingia katikati kama bima wa
malipo kwa kuhakikisha anamjua vyema Muuzaji(Seller) ambaye
ndio mlipwaji
Mlipaji aka Mnunuzi(Buyer) aliyeko Manzese hamlipi direct mlipwaji
aka Muuzaji(Seller) aliyeko Hong Kong,
Anachofanya Mnunuzi(Buyer) anampa ruhusa Pay Pal atoe pesa kwenye
Acc yake ya bank kutumia Master/Visa kisha amlipe Muuzaji(Seller)
Kwakuwa Pay Pal anakuwa amechukua dhamana ya malipo ya mauziano yenu
anawajibika kuhakikisha Muuzaji(Seller) ana bidhaa kweli anayouza na
anaaminika atatuma kwa Mnunuzi(Buyer) kile alicho tangaza,....Fail to
do so basi Pay Pal atawajibika kumrudishia Mnunuzi(Buyer) pesa yake,
na baada ya hapo Pay Pal kushirikiana na ebay ndio watao mtafuta na
kumbana Muuzaji(Seller) kwa utapeli alioufanya lakini wewe utakuwa
tayari umerudishiwa pesa yako iwapo watajiridhisha kuna uvunjifu wa
makubaliano.
Siku hizi biashara zimerahisishwa sana na maendeleo ya mtandao wa
intaneti unaowezesha watu kuuza na kununua vitu na huduma kupitia
mtandao. Kwa sababu ya maendeleo haya, mara nyingi tunapokuwa tunatumia
mtandao wa internet tunakutana na vitu mbali vizuri kama vile software,
vitabu, nguo, saa, magari au hata kozi ya kusoma kwenye mtandano.
Mara nyingi vitu hivi huwa na bei nzuri sana ambayo huvutia kununua.
Shida kubwa na yenye mantiki inayojitokeza ni usalama wa pesa zetu na
akaunti zetu za benki tunapofanya manunuzi kwenye mtandao. Mimi binafsi
ni mnunuaji wa kwenye mtandao hivyo nitakwenda kuelezea vitu vya muhimu
vya kufanya kabla hujatoa namba ya kadi yako ya benki kwenye matandao.
1. Tafuta Debit card au Credit card
Debit card ni kadi inayokuwezesha kununua vitu kwenye mtandao kwa
kutumia pesa iliyo kwenye akaunti yako ya benki. Na Credit card
inakuwezesha kununua kwa kukopa kwenye benki unayotumia halafu
wanakukata kidogokidgo kwenye mshahara wako au namna yoyote ambayo
mtakubaliana na benki. Kadi hizi ni kama Tembo card visa na Tembo card
master card za CRDB Bank;
benki zingine kama NBC, Stanbic Bank na BARCLAYS Bank pia zinatoa Kadi
Za namna hiyo. Baada ya kupata kadi yako unatakiwa uende kwenye benki
yako wakairuhusu kuweza kufanya manunuzi kwenye mtandao.
2. Jiunge na tovuti ya Paypal www.paypal.com
Paypal ni tovuti inayoongoza duniani kwa kusimia malipo ya kwenye
mtandao. Kazi yake kubwa ni kutunza taarifa zako muhimu za benki ili
wamachinga wa kwenye mtandao wasizizoee hovyo. Hivyo basi ukitumia
paypal, unasajili na kuweka namba yako ya visa au master card.
Baada ya hapo unaweza kuweka pesa kwenye account ya paypal au ukaziacha
kwenye akaunti yako ya benki. Unapofanya manunuzi Yule muuzaji anapewa
pesa na Paypal sio wewe moja kwa moja ili kulinda taarifa zako za benki.
3. Nunua kwenye tovuti iliyo na mfumo wa kutuma taarifa zako kwa usalama.
Kwa ajili ya usalama kuna teknologia inaitwa SSL(Secure Socket Layer).
SSL inafanya kazi ya kusafirisha taarifa zako katika hali ya mkanganyiko
ili mtu yoyote mhalifu asiweze kuzielewa, zikifika zianaundwa tena ili
muuzaji aweze kuzielewa.
Teknologia hii inatumika pia kutuma email, blackberry wakiwa ni vinara
wa kutunia teknologia hii. Ili kujua kama tovuti inatumia hii teknologia
utaona alama ya kufuli kwenye anuani ya tovuti husika ikishafunguka.
Angalia kwenye sehemu ya kuandikia anuani, kushoto au kulia.
4. Tumia tovuti inayoaminika
Unaponunua kitu kwenye mtandao kwanza kabisa hakikisha hiyo tovuti
inafahamika, kama haifahamiki hakikisha kuwa imethibishwa na na
mashirika yakuhalalisha biashara za kwenye mtandao kama BBB (Better
Business Bureau), utaona nembo ya haya mashirika chini kwenye tovuti ya
muuzaji.
5. Nunua kwa muuzaji anayekubaliwa na weteja wengi.
Utajuaje kama muuzaji anakubalika sokoni na anauzoefu wa kuuza vitu
kwenye mtandao? Rahisi! Kwa mfanounataka kununua saa Ebay au kitabu cha
electrniki (PDF) kwenye Amazon, chini ya hiyo bidhaa iliyoichagua utaona
maoni ya watu walionunua kabla yako.
Ni vizuri ukatumia muda wa kutosha kusoma maoni ya waru wengi kabla
hujaendelea za zoezi la manunuzi. Njia nyingine ya kupata maoni ya watu
ni kutumia tovuti kama Yelp, Google+, Yahoo directory au Yellow pages
iwapo muuazaji atakuwa amejiunga nazo.
6. Chagua namna ya kutumiwa mzigo wako.
Unatakiwa kuchagua namna kutumiwa mzigo wako ambayo itakuwa rahisi kwako
kuupata. Gharama za kutuma mzigo zitaoneshwa pale kwenye mtandao na muda
wa kufika kwa kila gharama. Kwa Tanzania unaweza kutumia DHL, UPS au
shirika lolote unaloliamini.
7. Hakikisha muuzaji anahudumia eneo ulilopo.
Baadi ya wauzaji huchagua nchi au miji wanayoweza kutuma mizigo na
wengine huuza dunia nzima. Taarifa hizi huwekwa chini ya bidhaa
unayotaka kununua , hii itakusaidia kuokoa muda kuondoa usumbufu usio wa
lazima.
Enjoy.