31.1.17

Fahamu jinsi ya kuhamisha mafaili yako kutoka kwenye iPhone kwenda kwenye Android bila kutumia iTune

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI.Wondershare TunesGo ni app inayokusaidia kumanage vitu vilivyopo katika simu yako ya Android na iOS. Unaweza ukahifadhi picha zako, muziki, video, apps, contacts pamoja na sms bila kati ya simu hizo mbili bila shida yoyote.

Uwepo wa Cloud Stores kama iCloud na Drive kunachangia sana katika kudhoofisha utumiaji wa programu za PC Suite kwa kuwa zinafanya shughuli zote kama zilizokuwa zinafanywa na PC Suites. Ila bado umuhimu wa programu hizi bado upo hasa pale unapohitaji kuhifadhi data zako katika kompyuta yako.
Wondershare TunesGo inaingia kati kama app bora zaidi inayotuwezesha kumanage vitu vyetu vyote vya muhimu katika simu bila kujali mfumo endeshi kama ni Android au iOS. Moja ya sababu kubwa itakayokufanya kuifurahia app hii ni uwezo wake wa kuhamisha data kutoka katika simu za iOS bila kutumia app ya iTunes.
                               main-screen-swahilitech
Usipate tabu kuhamisha namba kutoka simu yako moja kwenda nyingine pale unaponunua simu mpya au kuibiwa ya zamani, kila kitu cha katika simu yako ya awali utakikuta katika programu hii ya Wondershare TunesGo.