4.11.15

SOMA HAPA ANTI-VIRUS BORA ZAIDI KWA WINDOWS 10

BY net tamaduni

Karibu Net TAMADUNI. Windows 10 haitaingilia kazi mara kwa mara kukutaarifu kupakia‘Anti-virus’ kwenye mashine yako kama vile Windows 7 ilivyokuwaikifanya. Hii ni kwa sababu kuanzia Windows 8,  Microsoftwalifanyauamuzi wa msingi wa kuweka Anti-virus moja-kwa-moja kwenye mfumo
wao. Antivirus hii inaitwa Windows Defender na ni Antivirus ambayo
Microsoft wenyewe wanaitoa bure pamoja na WIndows mpya.



‘Je Windows Defender ni antivurus ni bora zaidi kwa usalama wa
kompyuta yako au la?’
Windows Defender 
WIndows Defender inatokana na Microsoft Security Essentials (MSE) na ni,
kwa maneno mengine, toleo la kisasa zaidi la MSE, ambayo ilikuwa ni
antivirus ya bure kabisa kwa ajili ya Windows 7. Kwa sasa, antivirus ya
Windows Defender inakuja pamoja na Windows na ni ngome ya kwanza kwa
kompyuta yako.
Je, Windows Defender Inatosha?
Unapoanza kutumia Windows 10, Windows Defender nayo huanza kufanya kazi
moja-kwa-moja na ku-scan kila programu unayofungua na kwa mpangilio wa
kawaida, inaji-sasisha yenyewe unapojiunga na mtandao. Kwa kawaida
Windows Defender haionekani wazi ikifanya kazi ila unaweza kupata ripoti
ya kina zaidi ya usalama wa kompyuta yako ukitaka kwa kuifungua Windows
Defender, kwa kuitafuta kwenye orodha ya programu zako kwenye ‘Start Menu'
                                     
Kiujumla, watalamu wengi mtandaoni husema kwamba anti-virus za Microsoft
zipo nyuma kidogo ya nyingine zenye ushindani, hata-hivyo, Windows
Defender ina faida lukuki.
Defender inakuja moja-kwa-moja na Windows na inafanya kazi kimya-kimya
(haina usumbufu wa matangazo mara kwa mara) na haitumii rasilimali
nyingi. Pia, haitatumia data zako za kwenye kivinjari, zinazotumika
kujaribu kutengeneza faida kama vile inavyofanywa na makampuni mengine
yanayotoa antivirus bure.

Windows Defender siyo mbaya sana kwa usalama kompyuta yako iwapo
ukizingatia mambo machache kama kusasisha kompyuta na kivinjari chako na
pia kuepuka kutumia programu hatarishi kama kiwezeshaji cha java (‘java
plugin’).

Kwenye matokeo ya AV-Test,Windows Defender ilipata0.5 / 6 kwa usalama, huku ikikamata 95% ya virusi na programu
hatarishi (“widespread and prevalent malware”) mnamo June mwaka huu,
pamoja na 85% ya virusi vya siku hadi siku

Ukilinganisha, BitDefender iliweza kakamata asilimia 100 na 100 ya
sampo, huku Kaspersky ikikamata asilimia 100 na 99. Kwa mantiki hiyo,
pamoja na utofauti kati ya matokeo hayo, Windows Defender bado ina
usalama wa kuaminika. Microsoft wenyewe wamekuwa wakisikika wakiweka
wazi kwamba dhumuni lao ni kushughulika na programu hatarishi na virusi
vinavyoathiri kompyuta nyingi na ni tofauti na watengenezaji wa
antivirus ambao wanashindana na virusi vya kila siku na hivyo kujiweka
katika mazingira mazuri ya kushinda majaribio yoyote.
                                                              
WIndows 10 pia ina usalama wa aina tofauti pia, ambao ulianza kutumikakatika Windows 8 kama SmartScreen filter ambayo inakuzuia kushusha na kupakia programu hatarishi, hatakama ukitumia antivirus tofauti na ya Microsoft. Chrome na Firefox nazohuwa na ‘Google’s Safe Browsing’, ambayo inakuzuia kushusha programu hatarishi.Kiujumla, Windows Defender inaweza kuwa sawa tu kwa watumiaji wakawaida. Hili ni pamoja na kuzingatia hatua chache za kujilinda. Ilani lakini, kama wewe ni mtumiaji wa programu ambazo siyo kutoka vyanzo vyakuaminika (kama torrent) na unafanya mambo mengine hatarishi kwa kompyuta yako, unashauriwa kutafuta antivirus nyingine yenye uwezo zaidi.
 
Tumia MalwareBytes Anti-Exploit Pia
Kama ziada unashauriwa sana kutumia programu maalumu ya kuzuia
mashambulizi yanayoelekezwa kwenye kivinjari na visaidizi vyake. Hivi
hulengwa sana na wadukuzi wa mtandao. MalwareBytes Anti-Exploit
ni mfano
wa programu kama hii, na ni ya bure ambayo unashauriwa kutumia.
MalwareBytes kazi sawa na programu ya Microsooft iitwayo EMET security tool
lakini ina utofauti wa kuwa rahisi zaidi kutumia na ina vipengele vingi
zaidi vya usalama. Hizi zana zinasaidia kuzuia mbinu nyingi
zinazojulikana za ki-udukuzi. MalwareBytes Anti-Exploit inaweza kuzuia
hata yale matatizo ya kiusalama ya Adobe Flash yanayosikika mara kwa mara.
                           
                                    

Windows Defender ikitumika sanjari na MalwareBytes Anti-Exploit ni
suluhisho tosha na la nafuu unaloshauriwa kutumia kufanya kompyuta ya
mtumiaji wa kawaida wa Windows 10 kuwa salama. Watu wanaotumia Windows
10 kwenye kompyuta za kiofisi zaidi wanaweza kuweka Windows Defender
ikishirikiana na Microsoft EMET, ila Windows defender na MalwareBytes
Anti-Exploit ni njema zaidi kwa kompyuta za kawaida. MalwareBytes
Anti-Exploit pia inaweza kutumika na anti-virus nyingine yoyote na
itakamata programu hatarishi na programu nyingine ambayzo hazihitajiki
(zinazolazimisha kujiweka zenyewe) na zile ambazo anti-virus huwa
hazikamati.
Lakini Antivirus Ipi Ni Bora zaidi?
Sawa, labda hauja-ielewa Windows Defender sana na unataka kitu kingine
chenye jina kubwa.
Kwenye swali hilo kuna majibu mawili: Kama unatafuta anti-virus ya
kulipia, Kaspersky na BitDefender kwa kawaida huwekwa kati ya anti-virus
3 nzuri zaidikatika majaribio mengi ya antivirus.
Kama unatufuta antivirus ya bure, Windows Defender bado ni jibu tosha.
Bado kama moyo wako unaenda kwenye anti-virus nyingine unazojua za bure,
hakikisha antivirus hizo haziweki kitu kwenye kivinjari chako au
kukuwekea programu nyingine amabazo pengine hupendi au hutumii. Hivi
vyote huwekwa ili kulipia kile wanachosema kwamba ni bure (hakuna kitu
cha bure aisee, ni ujanja tu). Wanalipaje? Wanatumia data zinazopatikana
kwa wewe kutumia programu hizo zinazojilazimisha kwenye kivinjari au
kompyuta yako – kwa maneno mengine, wanauza data kuhusu unatumiaje
programu hizo.
Windows Defender itaacha kufanya kazi unapoweka anti-virus nyingine
kutoka kampuni tofauti na Microsoft na kujirudisha tena pale unapotoa
anti-virus tofauti. Windows Defender imetengenezwa kutokubughudhi.
 
Neno la Mwisho
Kwa antivirus yoyote utakayoweka, tegemea kwamba hautakuwa salama
asilimia 100. Kama umezoea kushusha na kupakia programu hatarishi, ipo
siku utaingia matatani. Kuweka antivirus bora ni jambo la kukupa amani
kwamba uko salama ila kama haufuati taratibu za matumizi salama ya
kompyuta – ni kazi bure. Na katika dunia ambayo, kirusi cha kuogopa
zaidi ni kile kisichojulikana kabisa kile kinacholenga kivinjari,
MalwareBytes Anti-Exploit inaweza kuwa kimbilio bora zaidi kwa usalama
wa kompyuta ya Windows 10 kuliko kukimbilia antivirus nyingine zaidi ya
Windows Defender.