Ni swala lisilopingika kwa sasa kuwa kampuni ya Google inaendesha
asilimia 70 ya maisha yetu ya kimtandao kwa sasa hasa kama wewe ni
mwanafunzi, mfanyakazi au mfanyabiashara unayetumia mtandao katika
kufanikisha mambo yako. Jaribu kufikiria kama Google isingekuwepo wewe
mwanafunzi wa sasa unayechukua shahada au diploma yako maisha
yangekuwaje.
Ni ukweli usiopingika kuwa huwezi kuepeka kabisa huduma kutoka google
kwa sasa, ukikosa kutumia Google Search utatumia Google drive, Google
Map, Google Docs, Google Wallet, You Tube au hata Smartphones ambazo
zinatumia mfumo endeshi wa Android.
Hebu tuangalie huduma hizo;